BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APIGA MARUFUKU WANAFUNZI KWENDA SHULE NA SARE ZILIZOCHANIKA

Picha ya maktaba ikimuonyesha Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki akimvalisha viatu mwananfunzi wa shule ya msingi Kiromo hivi karibuni.

 WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku wanafunzi kuvaa sare zilizochanika na kwenda shule bila kuvaa viatu na kuwataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanakula ili wasome.

Amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kibiti kuanza msako wa wanafunzi watoro wa shule ili wazazi wao wachukuliwe hatua.

Ametoa maagizo hayo juzi mjini Kibiti wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara alipokuwa ziarani mkoani Pwani.

Waziri Majaliwa alisema Serikali ya Awamu ya Tano imefuta ada kwenye shule za msingi na sekondari za Serikali kama hatua ya kuinua kiwango cha elimu na kuwataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha watoto hao wanasoma na si kukatisha masomo na kuolewa.

“DC kuanzia sasa anza msako wa watoto wote wasioenda shule ili wazazi wao wakamatwe na kuchukuliwa hatua zinazostahili. Serikali imetoa fedha ili watoto wetu wasome na ni marufuku kuozesha mtoto wa kike, mzazi ukihusika tunakukamata na kukufunga na wewe uliyeoa nawe ni jela, hatuna mzaha kwenye hilo,” alisema.

Akizungumzia mahitaji ya watoto hao shuleni, Majaliwa alisema hivi sasa mzazi amepunguziwa mzigo wa kulipa karo na michango mingi ambayo Serikali imetoa na kuwataka wazazi kutumia fedha hizo kuhakikisha watoto hao wananunuliwa sare, viatu na kupewa chakula ili wasome vizuri.

“Zile fedha mlizokuwa mnatumia kulipa ada na michango sasa zitumieni kununua sare na chakula cha watoto wenu, ni marufuku mtoto kwenda shule huku akipekua au akiwa amevaa sare zilizochanika,” alisema.

Alisema wazazi ni lazima wahakikishe watoto wao wanasoma. Aliwaonya wazazi wenye tabia ya kuozesha watoto kwa kuwakatiza masomo waache mara moja kwani kuanzia sasa atakayebainika kukatisha masomo ya mwanafunzi hususan wa kike, ajiandae kwenda jela miaka 30.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema watumishi watatu wa Idara ya Misitu aliowasimamisha kazi kupisha uchunguzi wataendelea kuwa nje ya kazi.

Pia, alimrudisha kazini Ofisa Misitu wa Wakala wa Misitu wa Taifa (TFS) wilayani Rufiji kwa kuwa ni mtumishi mpya na hakuhusika kwenye uvunaji holela wa misitu.

Hata hivyo, aliwataka wafanyabiashara wenye leseni za kuvuna magogo kwenda katika ofisi ya Halmashauri kukaguliwa uhalali wa leseni zao huku wakisubiri utaratibu mpya wa uvunaji mazao ya misitu.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: