SEKTA YA ELIMU NA AFYA VINARA WA VYETI BABDIA TANZANIA
IKIWA zimebaki siku mbili kabla ya kuanza uhakiki wa watumishi wa umma kwa kutumia mashine za kielektroniki, imebainika kuwa sekta ya afya ndiyo inayoongoza kuwa na watu wenye vyeti bandia.
Serikali inatarajia kuanza keshokutwa uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma ili kubaini wafanyakazi waliopata ajira bila kuwa na sifa na kwa kutumia vyeti bandia.
Uhakiki huo pia unataraja kubaini watumishi hewa zaidi, ambao serikali ya awamu ya tano ilianza muda mfupi baada ya kuingia madarakani
Uchunguzi uliofanywa na Nipashe kupitia vyanzo mbalimbali umebaini kuwa vinara hao wa vyeti vya kielimu na kitaaluma visivyo na sifa, maarufu zaidi kwa jina la vyeti feki, wako zaidi katika sekta hiyo ya afya, wakifuatiwa na sekta ya elimu.
0 comments:
Post a Comment