Madhara ya ung'oaji viti uwanja wa taifa yaviathiri vilabu vya Yanga na Simba baada ya mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara uliowakutanisha mahasimu hao mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam juzi.
Hivyo basi vilabu hivyo vitalazimika ama kuuomba uongozi wa "AZAM" kuweza kuutumia uwanja wao kwa michezo ya vilabu hivi au kuhamia viwanja vya mikoani kwa kuwa uwanja wa zamani al-maarufu shamba la bibi kwa sasa umefungwa na upo kwenye ukarabati wa kurekebishwa nyasi za bandia kutokana na kupatwa kwa uchakavu mkubwa.
Wakati huo huo ukusanyaji, uhesabuji na upigaji wa tathmini ya viti vilivyong'olewa juzi na wanazi wakuu wa klabu ya simba sasa hesabu yake imekamilika mchana wa jana na klabu ya simba kukutwa na hatia na kuamriwa na serikalini kulipa Tsh 493 Milioni sawa na hasara ya viti 1781 vilivyong'olewa na kuvunjwa.
Yaani iko hivi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezifungia rasmi timu za Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka pale zitakaporuhusiwa tena na Serikali. Nape ametoa amri hiyo jana Jumapili ikiwa ni siku moja baada ya mashabiki wa klabu ya Simba, kung'oa viti vilivyopo kwenye majukwaa ya uwanja huo kwa kile walichokidai kupinga uamuzi wa Refa, Martin Saanya aliyechezesha mechi hiyo.
"Simba na Yanga hawatoutumia tena uwanja huu mpaka pale Serikali itakapoona kuwa mazingira yanaruhusu," alisema Nape.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / michezo /
slider
/ VILABU VYA SIMBA SC NA YANGA SC ZAGEUKA KUWA WATUMWA LIGI KUU TANZANIA BARA 2016/2017
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment