BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ALIYECHOMA MOTO KITABU KITAKATIFU CHA QURAN AANGUKA MAHAKAMANI


Mshtakiwa namba moja kati ya sita wanaokabiliwa na Kesi ya Jinai Namba 48 ya Mwaka 2016, Rashid Ausi (75), ameanguka kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.


Kutokana na tukio hilo, Hakimu wa Mahakama hiyo, Majinge Kusaga, aliahirisha kesi hadi Novemba 21, mwaka huu ambapo upande wa mashtaka utatoa maelezo yake.


Baada ya mshtakiwa huyo kupandishwa kizimbani, alianza kunyong’onyea na kunyoosha mkono ili aruhusiwe kuzungumza na baada ya kuruhusiwa, alizungumza kwa tabu na kusema anataka kulala, baada ya muda mfupi alianguka chini.


Mshtakiwa huyo alibebwa na kulazwa pembeni nje ya mahakama, baadaye alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


“Nalazimika kuahirisha kesi hii hadi Novemba 21, mwaka huu, kutokana na mwenzetu mmoja kukumbwa na maradhi, naomba turudi tena siku hiyo,” alisema Hakimu Kusaga.


Awali washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo wakituhumiwa kuchoma Kitabu cha Quran Tukufu ambacho hutumiwa na waumini wa Kiislamu, kuharibu mali na kumuita ndugu yao wa karibu mchawi.


Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya kosa hilo katika Kijiji cha Ngwinde, Kata ya Litola, wilayani humo ambao ni Ausi, Shazir Rashid (31), Rashid Nchimbi (35), Abdalla Nchimbi (56), Kanuti Nchimbi (53) na Juma Ndembo (36).


Umati mkubwa wa watu hasa waumini wa Kiislamu walijitokeza kuhudhuria kesi hiyo ili, kusikiliza mwenendo wake.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: