BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ALIYENG'OLEWA KWENYE UKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI (DCI) SASA AWA KATIBU TAWALA WA MKOA WA KAGERA


RAIS John Magufuli amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera. Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari jana, ilisema uteuzi wa Athuman unaanza mara moja.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi katika taasisi tano za Serikali.

Ilisema Rais Magufuli amemteua Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na kwamba uteuzi huo umeanza Novemba 16, mwaka huu.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa Rais amemteua Dk Jones Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na amemteua Sylvester Mabumba kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kwamba uteuzi huo umeanza Novemba 17, mwaka huu.

Iliendelea kusema kuwa Rais Magufuli pia amemteua Profesa Patrick Makungu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO) na uteuzi umeanza Novemba 16, mwaka huu na kuwa amemteua Martin Madekwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi ambapo uteuzi wake umeanza Novemba 17, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais amemteua Profesa Raphael Chibunda kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki Tanzania (TPRI) na uteuzi huo umeanza Novemba 17, mwaka huu.Habarileo
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: