BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ASKARI POLISI WAWILI WAFUKUZWA KAZI KWA KUWATESA WANAFUNZI KIDATO CHA NNE MBEYA


Kamanda wa Polisi wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari

POLISI mkoani Mbeya imewafukuza kazi askari wake wawili kutokana na kuwafanyia vitendo vinavyokwenda kinyume cha maadili wanafunzi wa kike wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Isuto iliyopo kijiji na kata ya Isuto, tarafa ya Isangati Wilaya ya Kipolisi Mbalizi mkoani hapa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Naibu Kamishna wa Polisi, Dhahiri Kidavashari, askari waliofukuzwa kazi kuwa ni Konstebo Petro Magana wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya na Konstebo Lucas Ng’weina wa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi.

Alisema jana kuwa Polisi ilianza ulinzi wa mtihani wa kitaifa wa kuhitimu kidato cha nne mwaka huu katika shule mbalimbali za Mkoa wa Mbeya, lakini katika kazi hiyo inayoendelea ya ulinzi wa mtihani kuna changamoto zilijitokeza.

Alisema Novemba 4, mwaka huu saa 5:30 usiku huko katika shule ya Isuto, askari hao walituhumiwa kuwafanyia vitendo vibaya kinyume cha maadili wanafunzi wa kike wa kidato cha nne wa shule hiyo.

“Inadaiwa kuwa, askari hao kwa pamoja wakiwa kwenye ulinzi wa mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne 2016 waliwatoa kwenye hosteli wanafunzi wa kike kwa kile walichodai kupiga kelele,” alieleza Kamanda Kidavashari na kuongeza: “Baada ya kuwatoa wanafunzi hao, waliwapeleka eneo la kufoleni na kuanza kuwapa adhabu mbalimbali ambazo ni kupiga push up, kuruka kichura, kushika masikio na kuwachapa viboko sehemu za makalio vitendo vilivyowasababishia maumivu makali na kusababisha baadhi ya wanafunzi hao wa kike kuondoka na kurudi majumbani kwao.”

Alisema kutokana na vitendo hivyo, Mkuu wa Shule hiyo, Rose Dihembe alitoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya uliochukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kusikiliza malalamiko ya wanafunzi na kuwaondoa askari waliolalamikiwa ambao baadaye walichukuliwa hatua za kinidhamu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: