BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DONALD TRUMP AMSHINDA HILARY CLINTON UCHAGUZI MKUU WA URAIS MAREKANI


Donald Trump alipakia picha hii kwenye Twitter, yake, mgombea mwenza wake na jamaa na marafiki wakifuatilia matokeo New York.

Donald Trump amemshinda Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.

Bi Clinton amempigia simu Trump kumpongeza kwa ushindi wake.

Trump alikuwa ameshinda majimbo mengi muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda.

Alikuwa ameshinda Ohio, Florida, na North Carolina, ingawa Bi Clinton alishinda Virginia.

Kwa sasa Trump ana kura 265 za wajumbe na Clinton 218 kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.

Lakini mgombea wa Republican Trump ameshinda majimbo mengi ya kusini mwa Marekani naye Bi Clinton akashinda majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa makadirio ya shirika la utangazaji la ABC News.

Kama ilivyotarajiwa, Trump ameshinda katika ngome za Republican katika majimbo ya Alabama, Kentucky, South Carolina, Nebraska, Indiana, West Virginia, Mississippi, Tennessee, Oklahoma na Texas, ABC News wanakadiria.

Trump pia anakadiriwa kushinda Arkansas, Kansas, North Dakota, South Dakota, Montana na Wyoming.

Shirika hilo linakadiria Bi Clinton atashinda ngome za Democratic majimbo ya New York, New Jersey, Connecticut, Massachusetts, Maryland, Vermont, Delaware, Illinois, Rhode Island na District of Columbia.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment