BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

FBI WAANGUSHIWA LUNDO LA LAWAMA KUSHINDWA KWA URAIS HILARY CLINTON UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI


Aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais wa Marekani kwa tikiti ya Chama cha Democratic Hillary Clinton, amesema kwamba kushindwa kwake ghafla katika uchaguzi uliyopita, kulichangiwa pakubwa na hatua ya mkurugenzi wa shirika la kijesusi la Marekani FBI, James Comey kutangaza uchunguzi mpya wa sakata ya barua pepe dhidi yake muda mfupi kabla ya uchaguzi.

Bi Clinton amewaambia wafadhili wa chama chake kwamba hatua ya Comey ilisambaratisha kampeini yake, licha ya uchunguzi huo kutompata na hatia.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kijasusi nchini Marekani FBI James ComeyMkurugenzi mkuu wa shirika la kijasusi nchini Marekani FBI James Comey  

Mwandishi wa BBC nchini Marekani hata hivyo amesema wengi wanahisi kuna msururu wa sababu zilizomfanya Donald Trump kumshinda katika uchaguzi huo.

Maelfu ya waandamanaji walifanya maandamano kwa siku nne mfululizo dhidi ya rais mteule Donald Trump.

Mjini New York ,maafisa wa polisi waliwazuia waandamanaji waliojaribu kukaribia bustani ya Union Square.

Wengine walielekea katika jumba la Trump Tower, nyumbani kwa  Trump pamoja na makao makuu ya biashara za Trump.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment