BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JAMBAZI AHUKUMIWA ADHABU YA KUCHAPWA VIBOKO 12 BAADA YA KUMPORA SISTER KANISA



MAHAKAMA ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora imemhukumu Peter John (30) kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 12 baada ya kupatikana na kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha kumwibia mtawa wa kanisa Katoliki mjini Igunga.

Akitoa hukumu hiyo mwishoni mwa wiki, Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Igunga, Leonard Nkola alisema mahakama imetoa adhabu baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Alisema kitendo kilichofanywa na mshitakiwa huyo kimekuwa kikilalamikiwa na serikali na hivyo mahakama ina wajibu wa kuwarekebisha watu wa aina hiyo ili jamii iwe salama.

Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi Igunga, Frank Matiku aliiambia mahakama mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Igunga, Leonard Nkola, kwamba Agosti 7, mwaka huu, saa tano na dakika 45 usiku katika Mtaa wa Mwanzugi, mshtakiwa aliiba fedha Sh 120,000 mali ya mtawa Alime Nisente wa Parokia ndogo ya Kanisa Katoliki iliyoko Mtaa wa Mwanzugi.

Aidha, Mwendesha Mashitaka alifafanua kuwa mshitakiwa kabla ya kuiba na baada ya kuiba vitu hivyo alitumia panga kumtishia mtawa huyo ili kujipatia mali hizo.

Matiku alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume cha kifungu 287 A cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 mapitio ya mwaka 2003 Sheria Namba 3 ya mwaka 2011.

Baada ya mshitakiwa kusomewa mashitaka yanayomkabili alikana mashitaka na ndipo upande wa mashitaka ulipeleka mahakamani mashahidi sita akiwemo mlinzi ambaye alimtambua mshitakiwa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: