BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AJALI YA NOAH NA LORI YAUA WATU 18 SHINYANGA

Picha ya maktaba gari aina ya Noah ikiwa imepata ajali 

Watu 18 wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika kijiji cha Nsalala Mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo iliyohusisha gari ndogo aina ya Toyota Noah na lori la mizigo ilitokea juzi saa 1:30 usiku baada ya dereva wa Toyota Noah iliyokuwa ikitoka Nzega kwenda Tinde mkoani Tabora, Seif Mohamed (32), kujaribu kuyapita magari mengine na kugonga uso kwa uso na lori lililokuwa likiendeshwa na Aloyce Kavishe, mkazi wa jijini Dar es Salaam. 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne alisema polisi inawashikilia madereva wote wawili kwa mahojiano na hatua za kisheria zitachukuliwa baada ya upelelezi kukamilika.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: