BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KLABU YA SABASABA UNITED FC YAPATA UHONDO WA LIGI DARAJA LA PILI TANZANIA BARA 2016/2017

Juma Mtanda, Morogoro
Timu ya soka ya Sabasaba United FC amepata ushindi wa kwanza ikiwa pungufu mbele ya Mkamba Rangers zote za Morogoro baada ya kuizamisha kwa bao la mkwaju wa adhabu ndogo katika mchezo wa ligi daraja la pili Tanzania bara 2016/2017 uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa jamhuri mkoani hapa.

Mshambuliaji, Gamba Iddy aliifungia timu yake “maarufu wauza mitumba” bao pekee dakika ya 68 kwa mpira wa adhabu ndogo baada ya yeye mwenyewe kuangushwa nje ya 18 na kupiga mpira kiufundi ulioenda kujaa kimiani huku kipa wa Mkamba Rangers, Amily Kiluwile akiwa hana la kufanya.

MTANDA BLOG ilishuhudia katika dakika ya 41, nahodha wa Sabasaba United, Iddi Ramadhan alizawadiwa kadi nyekundu na mwamuzi, Hashim Mketo kutoka Dar es Salaam baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa mchezo usio wa kiungwana uliopelekea Mkamba Rangers FC kucharazwa kwa bao 1-0.

Baada ya Sabasaba United kucheza pungufu kwa dakika 27, vijana hao wanaofundishwa na kocha mkuu, Amiri Ibrahim ilitandaza soka safi na mashambulizi makali ambapo dakika hiyi ya 41 mshambuliaji Hashim Mketo aliangushwa nje ya 18 na mpira wa adhabu yake kuzaa bao hilo pekee na ushindi.

Katika mchezo mwingine wa ligi daraja la pili uliofanyika kwenye uwanja huo huo wa jamhri mwishoni mwa wiki, timu ya Burkina FC ilishindwa kufurukuta mbele ya Changanyikeni ya Dar es Salaam na kujikuta wakipoteza kwa kutandikwa bao 1-0.

Bao la Changanyingine FC lilifungwa kiufundi na, Khalifu Khalifa dakika ya 23 kwa mpira wa kona uliochongwa na kwenda moja kwa moja na kutua kwenye nyavu za Burkina FC na kujikuta wakipoteza mchezo huo.

Burkina FC inayonolewa na mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba ambaye ni kocha mkuu, Ulimboka Mwakingwe ilipoteza nafasi nyingi za wazi za kujaza mpira kimiani kutokana na kushindwa kutumia vyema nafasi walizopata na kuifanya Changanyikeni FC kuibuka na ushindi huo wa bao 1-0.


Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment