BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAMBO YALIYOACHWA NA KUPIGWA MUHURI USIOFUTIKA NA SAMWEL SITTA WAKATI WA UHAI WAKE


Na
Ndimi Luqman Maloto  

Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta ameshatimiza ile ahadi ya Mungu na wanadam kuwa kila nafsi itaonja mauti.

Muhimu sasa ni kumuombea heri katika sura ya maisha baada ya kifo.

Funzo la karibu kuhusiana na kifo cha Sitta ni maisha yenye kuacha alama.

Sitta ameacha alama; Ujenzi wa Daraja la Selander. Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam (sasa Julius Nyerere International Airport). Kuanzisha ATC na kusomesha marubani wa kwanza Tanzania. Kuanzisha Posta na Simu, Mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Alama ziendelee; Kuchora mstari wa siasa za kisasa ndani ya Bunge. Kuupa sauti upinzani bungeni. Kutengeneza mazingira rafiki ya uwekezaji Tanzania, alipokuwa mkurugenzi mtendaji wa TIC. Ujenzi wa nyumba za Serikali Dodoma. Ujenzi wa Barabara Dodoma to Moro kwa fedha za ndani. Ujenzi wa Barabara ya Makambako to Songea fedha za Serikali.

Yapo mengi ila naweka kituo.
Tunza hii kichwani; Tuishi tukiwa na shabaha ya maisha ili siku tukiondoka tuache alama. 


Kuacha alama siyo kuacha watoto yatima. Ni kuacha vitu vyenye kuitambulisha thamani yako ya kuishi hapa duniani. Hata ukiwa haupo, watu wazienzi, wazifurahie na kuzitukuza nyakati za uhai wako.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment