MAAFISA WA POLISI 14 NA WASHAMBULIAJI 41 WAFARIKI DUNIA KATIKA MAPAMBANO YA RISASI ZA MOTO
MAOFISA 14 wa polisi na washukiwa wa ushambuliaji 41 wamethibitishwa kufa katika mapambano baina ya vikosi viwili vilivyopo Wilaya ya Kasese mkoani Rwenzori juzi.
Milio ya risasi ilisikika wilayani Kasese juzi jioni na iliendelea hadi usiku wakati maofisa wa polisi walipokuwa wakiwasaka watu wenye silaha walioshukiwa kuwashambulia polisi.
Mapigano yalitokea katika sehemu tofauti za wilaya na kusababisha gari la poliai kuchomwa moto huko Kagando, Bukonzo Magharibi.
Msemaji wa polisi, Andrew Felix Kaweesi aliwaambia wanahabari mjini hapa jana kuwa mbali ya polisi hao 14 na watuhumiwa 41 wa Rwenzori, askari wawili wa jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) walijeruhiwa.
“Tunaamini mashambulizi haya yana harufu ya kisiasa na hadi sasa tumekamata viongozi wa 15 wa genge hili. Huu si uanamgambo bali machafuko ya kihalifu,” alisema.
Aidha tarifa nyingine zinasema wapiganaji hao ni wafuasi wa Mfalme wa Jamii ya Bakonzo iliyopo mpakani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo imekuwa kwa muda mrefu ikikabiliana na jamii ya ufalme wa Tori eneo hilo.
Miaka kadhaa ya mapigano ilihitimishwa mwaka 1982 kukiwa na makubaliano ya kuwepo na uhuru huku Rais Museveni akizitambua rasmi falme hizo mwaka 2009, lakini wasiwasi umezidi kutanda.
0 comments:
Post a Comment