BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI WAMZUIA MWANAFUNZI KUINGIA DARASA LA KUSOMA MASOMA YA UWAKILI KWA KUVAA SKETI FUPI.


Mwanafunzi mmoja nchini Uganda, Joaninne Nanyange amechapisha ujumbe mrefu katika mtandao wake wa Facebook akilalamika vile alivyozuiwa kuingia katika mlango wa darasa lake la chuo kikuu siku ya Jumatano na wanawake wawili mmoja akiwa amevalia magwanda ya polisi.

Anasema askari huyo alimtaka kuvuta sketi yake chini hadi mwisho.

''Nilicheka kwa sababu ombi lake halikueleweka.Alisisitiza hivyo basi nikamwambia hapo ndipo mwisho na hakuna vile ningeweza kuivuta hadi chini''.

Ni hapo ndipo alipoelezewa kuwa sketi yake ni fupi na kwamba hangeweza kujiunga na wenzake katika darasa la kusomea uwakili.

Hatahivyo kitivo cha uwakili mjini Kampala kimesema kuwa hakijapokea malalamishi rasmi kuhusiana na tuki hilo.

Lakini msemaji wa kituo hicho amesema kuwa kuna maadili ya mavazi na kwamba wanawake wanafaa kuvaa sketi zinazofika magotini.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: