BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKUU WA WILAYA APIGA MARUFUKU WANANCHI KULA PIPI WAKATI WAKISAFIRI NA GARI TANZANIA.

Pichani ni picha ya pipi aina ya loto ikiwa imefungwa na kifunga chache maridadi lakini sio inayozungumziwa katika habari hii. Picha ya maktaba.

MKUU wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, amewatahadhirisha wananchi kutodhubutu kupewa pipi na mtu yeyote ndani ya gari binafsi au basi la abiria.

Amesema baadhi ya pipi hizo hupakwa dawa za kulevya na kusababisha kupoteza fahamu.

Amesema tayari madhara ya ulaji wa pipi yalimkuta mtumishi mmoja wa Serikali ambaye alipewa pipi ndani ya basi na kujikuta akizinduka akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekeo Toure, akipatiwa matibabu.

Tahadhari hiyo aliitoa alipozungumza na wananchi wa Kata za Igoma na Kishili kuhusu mambo mbalimbali ya ulinzi na usalama ndani ya wilaya ya Nyamagana.

Tesha ambaye hakutaka kutaja jina lake la mtumishi huyo aliyekula pipi lakini alidokeza cheo chake kuwa ni mkurugenzi.

Alisema alipewa pipi na abiria mwenzake aliyekuwa jirani na muda mfupi alisinzia na kupoteza fahamu.

“Naombeni wananchi tuwe na tahadhari sana juu ya ulaji wa vitu ndani ya vyombo vya usafiri, hili nalisema wazi kwani limekuwa likijitokeza.

“Hivi karibuni kuna mtumishi mmoja alikuwa anasafiri ambako alipopewa pipi na abiria mwenzake kumbe ilikuwa imepakwa dawa za kulevya.

“Mtumishi huyo ambaye tena ni mkurugenzi alijikuta akizindukia Sekeo Toure, hajui alifikishwa vipi katika hospitali hiyo.

“Epukeni ulaji wa pipi pia kwa sababu umekuwapo utapeli kwa njia ya simu nao umeendelea kutikisha nchi na watu kuibiwa mamilioni ya fedha,”alisema.

Tesha alizungumzia suala la wana wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba akiwaonya wazazi watakaoshindwa kuwapeleka kuanza kidato cha kwanza watafikishwa mahakamani.

Alisema ifikapo Januari 31, 2017 ataanza ziara ya kutembelea shule zote ndani ya Nyamagana kubaini wanafunzi walioshindwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza na kuwachukulia hatua wazazi wao.

Wananchi wa Igoma na Kishili walimweleza DC kwamba kumekuwapo na kero ya kukatika daraja la Fumagila linalounganisha wilaya za Misungwi na Nyamagana na kusababisha wananchi kushindwa kwenda shule hasa mvua inaponyesha.

Akitoa majibu, alisema tayari Serikali imetenga Sh milioni 300 kwa ajili ya kujenga daraja la Fumagila na kuwataka wazazi kuwasindikiza wanafunzi na kuwavusha upande wa pili mvua inaponyesha.MTANZANIA
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: