BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BLACK VIBA FC YAIFUMUA MZINGA FC LIGI YA MKOA WA MOROGORO.

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Mzinga FC, Galus Ndenga akijaribu kumiliki mpira wakati mchezaji wa Black Viba FC, Daud Milandu akiwania mpira huo na mwamuzi wa mchezo huo, Kassim Salehe akishuhudia tukio hilo katika ligi daraja la tatu hatua ya sita bora mkoa wa Morogoro ambapo katika mchezo huo Mzinga FC ilitandikwa bao 1-0. Juma Mtanda.


Juma Mtanda, Morogoro.
Timu ya soka ya kikosi cha jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mzinga FC kimesambaratishwa na kutupwa nje kuwania ubingwa wa ligi daraja tatu mkoa wa Morogoro hatua ya sita bora 2016/2017 baada ya kukubali kukung’twa bao 1-0 na Black Viba FC katika mchezo mkali uliofanyika kwenye uwanja wa jamhuri mkoani hapa.

Mshambuliaji wa Black Viba FC, Farijala Mustapher alizima ndoto za Mzinga FC kusonga mbele kuwania ubingwa huo baada ya kufunga bao dakika ya 22 akipokea pasi ya, Hamis Mkopi aliyefanya kazi ya ziada ya kuwatoka wachezaji wa Mzinga FC kabla ya kutoa pasi hiyo iliyozaa bao pekee.

Juhudi za wachezaji wa Mzinga FC kutaka kusawazisha bao hilo na kupata la ushindi ziligonga mwamba kufuatia kukutana na vikwazo kutoka safu ya ulinzi ya Black Viba FC na kipa, Gumbo Issa lakini nafasi walizopata washambuliaji wao walishindwa kuzitumia kufunga na kujikuta wakitandikwa bao 1-0.

Mwamuzi wa mchezo huo, Kassim Salehe aliyechezesha vyema paambano hilo alimlamba kadi nyekundi mchezaji wa Black Viba FC, Emmanuel Mbelwa dakika 70 kwa kuonyeshwa kadi mbili za njano huku mchezaji wa Mzinga FC, Isihaka Shomari naye akilambwa kadi nyekundu dakika ya 79 baada ya kumchezea vibaya, Hamis Mkopi.

Kutokana na matokeo hayo Mzinga FC imeungana na Gairo DC FC kuaga ligi hiyo na kuziacha Shupavu FC, Black Viba FC huku timu za Moro Kids FC na Kizuka FC zikikamilisha ratiba katika mchezo wa leo (jana) saa 10 jioni zikisonga mbele.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Katibu mkuu mtendaji wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA), Charles Mwakambaya alieleza kuwa baada ya kumalizika kwa hatua ya sita bora hatua itayofuata, timu hizo kucheza nusu fainali na fainali.

“Hatua ya sita bora ya ligi hii daraja la tatu inamalizika leo (jana) kwa mchezo wa kukamilisha ratiba ya mchezo kati ya Moro Kids FC na Kizuka FC ili kupata timu nne zitakazoingia nusu fainali kisha kupata timu mbili za kucheza fainali na hatimaye kupata bingwa wa mkoa wetu.”alisema Mwakambaya.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: