BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NJIA TANO ZA KUPITIA ILI KUWA TAJIRI NDIO HIZI

WAKATI idadi kubwa ya vijana wakihangaika na maisha kutafuta maendeleo, mtaalamu wa Diplomasia na Uchumi, Joel Nanauka amegundua mbinu kuu tano ambazo mtu akizitumia atauaga umasikini. 

Mojawapo ya mbinu hizo, amesema, ni mtu kugundua kipaji alichowezeshwa na Mungu kuliko kutegemea elimu ya duniani.

Nanauka aliyasema hayo wakati akizindua kitabu chache kiitwacho ‘Timiza Malengo yako’ alichokiandika kwa miaka mitatu kinachoelezea mbinu 60 walizotumia matajiri na watu mashuhuri ulimwenguni, ambazo zimewapelekea kuwa na mafanikio makubwa.

Nanauka ambaye aligombea Ubunge jimbo la Mtwara mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwenye uchaguzi mwaka jana, alitaja mbinu nyingine kuwa ni mtu kufanya kazi ambayo anaipenda mwenyewe na siyo kulazimishwa.

“Watu wengi wanafanya kazi ambazo hawazipendi," alisema Nanauka. "Utakuta mtu ikifika Jumatatu anachukia kuliko inapofika siku za mwisho wa wiki."

"Hiyo ina maana kuwa watu hao hawapendi kazi zao.”

Nanauka alisema ili mtu afanikiwe ni lazima afanye kitu ambacho anakipenda kutoka moyoni, hali ambayo itamwezesha mtu huyo kufanya kazi hiyo kwa ubora zaidi na kujipatia mafanikio.

Nanauka alitaja mbinu ya tatu kuwa ni mtu kutosubiri vitu vyote vikamilike.

Alisema watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wanasubiri mazingira yote yakamilike, akitolea mfano sababu inayotolewa na watu wengi ya ukosefu wa mtaji.

Alisema ili mtu afanikiwe siyo lazima awe na mtaji bali maarifa na watu waliosahihi, "ndiyo vitu vya muhimu vinavyohitajika.

“Utakuta mtu anasema siwezi kufanya hadi niwe na shahada, kwani watu wangapi wamefanikiwa bila ya kuwa na shahada?

"Wengine wanasema hawawezi kuanza kufanya biashara hadi wawezeshwe mtaji, siyo kweli kwani nguvu ya wazo ni kubwa zaidi kuliko kujiangalia una nini.”

Nanauka alisema mbinu nyingine ni kutokukata tamaa. Alisema watu wengi wanakata tamaa ya maisha mapema kwa sababu walishindwa.

Alisema aliyewahi kuwa Rais wa Marekani, Abraham Lincon aligombea nafasi hiyo mara nane na kukosa, alifanya biashara lakini hakufanikiwa.

Mbinu nyingine ni kujitambua. Alisema watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu hawajajitambua wao ni akina nani na wanatarajia nini.

Alifafanua kuwa watu wanakuwa wanasoma darasa moja, wametoka familia moja lakini mmoja anafanikiwa na mwingine hafanikiwi.

"Hiyo inatokana na mtu kutojitambua na kutokuwa na malengo ya baadaye." Nanauka alijitambulisha kuwa mtaalamu wa Diplomasia na Uchumi.Nipashe
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: