Rais mteule wa Marekani Donald Trump
alipokutana na Rais Barack Obama kwa mara ya kwanza ikulu ya White
House tangu ashinde uchaguzi, uadui kati yao ulijidhihirisha.Rais Obama naye alisema Mwanarepublican huyo hana sifa na uwezo wa kuwa kiongozi wa Marekani.
Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York, ambaye sasa ni rais mteule, kwa muda mrefu alitilia shaka uhalali wa habari kwamba Obama alizaliwa Hawaii, na alikejeliwa hadharani na Rais Obama.
Wawili hao walishauriana kwa zaidi ya saa moja afisi ya rais katika ikulu ya White House mnamo Alhamisi na walipojitokeza kwa wanahabari, walijaribu kuficha uadui kati yao.
Waliongea maneno mazuri kuhusu umoja na umuhimu wa kupokezana madaraka kwa amani lakini picha zilizopigwa zinaonesha jambo tofauti, ukiangalia sura na mikono.
Nikiangalia sana pale mbali, haya masaibu yote yatapita.
Fikira za Trump zinaonekana kuyumba.... labda kwa kukumbuka aibu iliyotokana na utani kuhusu kuzaliwa kwa Obama mwaka 2011.
Wanasalimiana lakini macho yako wapi.... tazama mdomo wa Trump
Tena, sasa Obama anamwangalia Trump.... lakini Trump anaamua, la hasha, SIWEZI kumwangalia machoni
Kupeana mikono kwisha sasa, na ni furaha sana kwa Trump .... lakini anaonekana kutoyaamini anayoyasema Rais Obama
Wawili hao walicheka wakati mmoja walipotaniana. Melania na Michelle pia walikutana, lakini hawakuonekana kuwa na matatizo
Melania Trump na Michelle Obama wakiwa ikulu ya White House.BBC

0 comments:
Post a Comment