BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI (TUCTA) LAMPIGA TEKE KATIBU MKUU WAKE


ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Nicholaus Mgaya, ameshindwa kutetea kiti chake baada ya kugaragazwa na Dk Yahaya Msigwa katika uchaguzi uliofanyika na kumalizika usiku wa manane kuamkia jana.

Dk Msigwa anatoka katika Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE).

Kiongozi pekee aliyefanikiwa kutetea nafasi yake katika uchaguzi huo wa jana ni Mweka Hazina wa shirikisho hilo James Kalanje.

Akitangaza matokeo hayo jana asubuhi, Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Uchaguzi huo, Dk Salma Chande, alisema wajumbe wa mkutano huo walipiga kura usiku kucha pasipo kutokea kwa vurugu za aina yoyote.

Kwa majibu ya matokeo hayo, mshindi wa nafasi ya Urais, Tumaini Nyamkokya alipata kura 161 wakati Makamu wake Qambos Sulle alishinda kwa kura 175.

Katika uchaguzi huo aliyeukwaa Katibu Mkuu Dk Msigwa alipata kura 180 akimshinda Mgaya aliyepata kura 152 na naibu wake akipata kura 179.

Nafasi ya kamati ya wanawake, Rehema Ludanga alishinda kwa kura 105 na katibu wake Mtui ameshinda kwa kura 92 Msimamizi wa uchaguzi huo alikuwa alitangaza kura za washindi tu na nafasi hizo zilirudiwa kura mara mbili kwa sababu mara ya kwanza washindi hawakupata asilimia 50 kama katiba inavyotaka.

Kutokana na matokeo hayo msimamizi huyo alimtangaza Tumaini Nyamghokya kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kuwa mshindi na kushika nafasi ya Rais wa Tucta akimrithi Gratian Mkoba aliyemaliza muda wake.

Aidha, Dk Chande alimtangaza Qambos Sulle kutoka Chama cha Walimu (CWT), kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tucta, Dk Msigwa (Katibu Mkuu), Kalanje (Mweka Hazina) na Rehema Ludenga kuwa Mwenyekiti Kamati ya Wanawake.

Aliwatangaza pia Noel Lotary kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO), Menson Mkwawa (CWT), Rehema Mbaga (Talgwu) na Marystella Kalwera, Kuwa wadhamini wa shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka mitano.

"Tunashukuru uchaguzi umemalizika bila kuwapo na figisu figisu yoyote, uongozi mpya umejulikana, sasa tunawaachia waliochaguliwa waendelee na majukumu yao mapya," alisema Dk Chande.

Alisema uchaguzi huo ulikuwa na ushindani mkali kwa vile wajumbe walipata shida ya kuwatambua viongozi watakaowafaa kutokana na wengi wao kufanana sifa.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Katibu Mkuu mteule wa shirikisho hilo, Dk Msigwa aliwashukuru wajumbe kwa kukesha ili waweze kupata viongozi bora watakaowafaa kuwatumika katika kipindi cha miaka mitano watakachokaa madarakani.

"Mmenichagua ili niwe Mtendaji Mkuu wa shirikisho, hivyo nawaahidi nitaongoza kwa kufuata kanuni, Katiba na sheria zilizopo ndani ya shirikisho letu," alisema Dk Msigwa.

Naye Rais mteule wa Tucta, Nyamghokya, aliwataka wanachama wanaounda shirikisho hilo kushirikiana ili kupata mafanikio makubwa zaidi.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: