BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIRI YA KUFUFUA VIWANDA YAFICHULIWA


Katibu mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Adolph Mkenda ametaja mambo sita ambayo yanafanywa na Serikali ili kufufua viwanda na kuimarisha sekta ya uwekezaji.

Mkenda ameyataja mambo hayo leo (alhamisi) kwenye mkutano wa kimataifa unaojadili mageuzi ya viwanda na kijamii nchini unaofanyika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM).

Mambo hayo ni uwepo wa amani ya nchi, kuendeleza miundombinu rafiki kwa viwanda, kuongeza kasi ya ufanisi ya utendaji kazi serikalini, kupitia kanuni na taratibu mbalimbali zinazokuwa ni bughudha kwa wawekezaji, kupunguza tozo na ada ambazo zimekuwa nyingi na kufungua fursa ya soko la kimataifa.

"Tunataka kupunguza hizi tozo, kodi na ada zisiwe nyingi, tutafanya kwa kurahisisha malipo yote yalipwe sehemu moja na si kulipa sehemu tofauti," amesema Mkenda. 


Mkenda ameongeza miundombinu rafiki ni ile ambayo itarahisha wawekezaji kuwekeza nchini ni kama barabara, umeme wa uhakika na maji ambayo humfanya mwekezaji kujenga kiwanda mahala popote nchini.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: