BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SPIKA MSTAAFU SAMWEL SITTA AFARIKI DUNIA UJERUMANI NA HUU NDIO UGONJWA ULIOSABABISHA UMAUTI WAKE

Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel Sitta (74) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani.

Mtoto wa marehemu, Benjamin Sitta amesema baba yake amefariki saa 10:00 usiku wa kuamkia leo.

‘’Nikweli mzee amefariki nchini Ujerumani akiwa anapatiwa matibabu, alipelekwa Alhamisi iliyopita na alikuwa anasumbulia na saratani ya tezi dume ambayo ilisambaa na kuathiri miguu na mwili mzima.

Benjamin amesema kuwa taarifa za mipango ya kusafirisha mwili zitatolewa baadaye.

Sitta alikuwa Spika wa Bunge tangu mwaka 2005 hadi mwaka 2010 na pia mbunge wa Urambo Mashariki.

Pia, alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na aliwahi kuwa waziri katika wizara mbalimbali kwa vipindi tofauti.

Alikuwa miongoni mwa wanachama zaidi ya 42 wa CCM waliochukua fomu za kugombea urais mwaka jana.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: