BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NYUMBA ZAIDI YA 700 ZAEZULIWA KWA UPEPO NDANI YA DAKIKA 30 TU

FB_IMG_1478439274060.jpegBaada ya tetemeko la Septemba 10 lililoacha vifo vya watu 17 na uharibifu mkubwa wa makazi na miundombinu kwenye Kanda ya Ziwa, lakini hasa mkoani Kagera, kaya 118 zenye watu zaidi ya 700 katika Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, zimekosa makazi, baada ya nyumba zao kubomolewa na nyingine kuezuliwa na mvua iliyonyesha kwa dakika 30 ikiwa imeambatana na upepo mkali juzi.

Tetemeko hilo lilielezwa kuwa na ukubwa wa 5.7 katika vipimo vya majanga hayo kimataifa, na kwa mujibu wa mtandao wa kompyuta wa earthquaketrack.com ndilo kubwa zaidi katika historia kutokea nchini katika miaka ya 2010.

Mvua hiyo ya juzi iliyoambatana na upepo mkali, ilinyesha usiku na kusababisha athari kadhaa, ikiwamo kuharibu mazao mashambani na watu watatu kujeruhiwa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: