BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UJERUMANI YATOA FEDHA ZA WAKIMBIZA WA TANZANIA

Picha ya maktaka wakionekana wakimbizi.

SERIKALI ya Shirikisho la Ujerumani na watu wa Ujerumani wametoa msaada wa fedha Euro milioni 11 sawa na Sh bilioni 26.4 kwa ajili ya kusaidia uendeshaji wa shughuli za wakimbizi nchini.

Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke alisema fedha hizo zitasimamiwa na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) pamoja na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

Balozi Kochanke alisema UNHCR watatumia fedha hizo kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali ambazo zinahitajika kwa wakimbizi waliopo nchini na baadhi ya fedha zitatumika kusaidia mahitaji ya chakula cha wakimbizi hao.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Michael Danford alisema hali ya chakula kwa wakimbizi inategemea wahisani kama Ujerumani, hivyo misaada hiyo itawawezesha kuishi na kupata mahitaji ya chakula.

“Kama mnavyojua wakimbizi wanakuja wakiwa hawana kitu chochote, wanaacha makazi yao hivyo wanahitaji msaada huo kwa kiasi kikubwa ili waweze kuendelea kuishi,” alisema Danford.

Akishukuru kwa msaada huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hasan Simba Yahya alisema wamekuwa wakiwakumbusha kuzingatia hali za wananchi wanaopokea wakimbizi kwa sababu hali zinakuwa si za kuridhisha na hivyo kufanya watoto kudumaa na hivyo kuathiri watoto.

“Kama serikali tutaendelea kubeba jukumu la kuhudumia wakimbizi kadri wanavyokuja kwa kuwa ni jukumu la kimataifa hivyo kubwa ni kuwakumbusha wahisani wakihudumia wakimbizi wasiishie hapo bali wakumbuke na jamii inayowapokea wakimbizi,” alisema Balozi Yahya.

Aliongeza, “wanaopokea wakimbizi watazamwe badala ya kuachwa kwa kuwa wanaathirika na uharibifu wa mazingira kwenye maeneo yao na pia hali ni mbaya ya usalama katika maeneo yao kutokana na kuja kwa wakimbizi wengi kwa wakati mmoja.

“Mtu anakuja anaingia hana chochote na ana watoto wana njaa, hivyo ataingia kwenye shamba lenye muhogo na hapo ndipo vurugu zinaanza, hivyo ili hayo yote yasitokee nguvu zielekezwe kwa watu wanaopokea wakimbizi katika maeneo hayo.”
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: