BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

USHINDI WA URASI MTEULE WA MAREKANI DONALD TRUMP WAPINGWA KILA KONA KWA MAANDAMANO

 

Na Geofrey Chambua.
BBC imetaarifu kwamba Maelfu ya watu wameandamana katika miji mbalimbali nchini Marekani jana kupinga ushindi wa Donald Trump wa chama cha Republican.

KWAMBA Mamia ya waandamanaji wanaompinga Trump walikusanyika nje ya jumba kuu la Bw Trump, Trump Tower eneo la Manhattan jijini New York Jumatano jioni, wakibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe "Not my president" (Si Rais wangu), pamoja na mabango mengine.

Kama Mzengezi mbobevu ninashawishika kuamini kwamba huenda watahitaji kufanya UCHECHEMUZI kwani ukakasi wao umejikita zaidi kwenye SERA NA MFUMO na si WIZI WA KURA.....

Mfumo wa uchaguzi Marekani
Hata ingawa Marekani inafikiria kuwa ndio nchi inayo ongoza katika masuala ya Kidemokrasia, mfumo wake wa kumchagua hauwashirikishi raia moja kwa moja kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo

Kila jimbo nchini Marekani lina wajumbe kutegemea na idadi ya wapiga kura (uwiano) katika jimbo hilo. Kuna jumla ya wajumbe 538 katika majimbo yote, katika midadi hiyo kuna wawakilishi 435, Maseneta 100 na kuna wawakilishi watatu kutoka Wilaya ya Columbia. 


Idadi ya wajumbe maalum katika kila jimbo ni sawa na idadi ya wabunge kutoka kwenye jimbo husika kwa mfano katika jimbo la California kuna wajumbe 55 kwa hiyo idadi hiyo ni sawa wabunge wake wanao wakilisha bungeni mjini Washington.

Mgombea urais atahitajika kupata angalau kura 270 za wajumbe maalum ili kuweza kushinda kinyang'anyiro cha urais nchini Marekani. 


Hadi kufikia sasa chaguzi 57 za urais zimefanyika nchini Marekani ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa mwaka 2000 wakati ambapo wagombea walikuwa Al Gore wa chama cha Democratic dhidi ya George W Bush wa Republican ambapo Bush aliibuka kuwa rais wa Marekani hata ingawa Al Gore ndie aliyepata kura laki 5 na elfu 40.

Zaidi alizopigiwa na wananchi wa Marekani lakini kwa kuwa hakupata idadi kubwa ya kura za wajumbe maalum basi hakuweza kuchukua hatamu za uongozi kutokana na mfumo wa uchaguzi wa Marekani ambapo katiba inawapa nguvu wajumbe maalumu kuamua ni mgombea yupi atakae iongoza nchi hiyo.

mifano ipo mingi na historia hii ni kubwa sana ila kula hizo chache

Wakosoaji wa masuala ya kisiasa wanaukosoa mfumo huo wa kuchaguliwa rais wa Marekani na wajumbe maalum, wanasema umepitwa na wakati na kwamba unastahili kubadilishwa kwa kufuata matokeo halisi ya kura zilizopigwa na wananchi. wanautaja kuwa kuwa unafedhehi mfumo mzima wa upigaji kura na hasa kwa wapiga kura wenyewe.

Kwa nyakati fulani, Televisheni ya CNN kwa upande wake imekiri kuweko upogo huo na kuripoti kuwa wananchi wengi wa Marekani hawapendezwi na mfumo wa kutochaguliwa rais wa nchi hiyo kwa kura za moja kwa moja za wananchi na wametaka sheria hiyo ifutwe kabisa katika katiba ya Marekani.

Wajumbe maalum wanapinga vikali tuhuma hizo
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment