BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE WA JIMBO LA KILOMBERO AITWA KUOKOA JAHAZI LA TIMU YA SHUPAVU FC MOROGORO.

 
Mbunge wa jimbo la Kilombero Chadema, Peter Lijualikali.

Juma Mtanda, Morogoro.
Mbunge wa jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali amepigiwa magoti na uongozi wa timu ya soka ya Shupavu FC ili kusaidiana na wadau mbalimbali kuipiga jeki timu hiyo kuwezesha upatikanaji wa Sh2.5mil.

Upatikanaji wa fedha hizo utasaidia katika maandalizi ya ligi daraja la tatu hatua ya nusu fainali ya kuwania ubingwa wa mkoa wa Morogoro 2016/2017 baada ya kukumbwa na ukata wa kuendesha timu hiyo mkoani hapa. 

Akizungumza na MTANDA BLOG wakati wa michezo ya ligi hiyo hatua ya sita bora uwanja wa jamhuri mjini hapa, Mhasibu wa timu hiyo, Fungo Lucian alisema kuwa uongozi unasaka fedha kiasi cha Sh2.5 mil na tayari wameandika barua ya kuomba fedha kwa mbunge wa jimbo hilo na wadau wengine ili kujikwamua kiuchumi.

Lucian alisema kuwa upatikanaji wa fedha hizo utasaidia katika matumizi mbalimbali ikiwemo chakula, malazi na usafiri wakati wa michezo ya nusu fainali pengine na fainali ambapo timu hiyo tayari imetinga nusu fainali ya ligi hiyo.

“Mimi ndiye mhasibu wa timu hii ya Shupavu FC na jioni hii (juzi) tunalazimika kusafiri usiku kurudi Ifakara kutokana na kukosa fedha za kulipia malazi, chakula na matumizi mengine muhimu ya timu ndio maana umefanyika uamuzi wa kurudi haraka ili kukwepa gharama nyingine.”alisema Lucian.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Methew Mtenga alisema kuwa Shupavu FC tayari imefuzu kuingia nusu fainali baada ya kushinda michezo yake ya hatua ya sita bora kwa kuzisambaratisha timu za Black Viba FC kuitandika bao 2-1 huku ikipata ushindi mwingine wa bao 2-0 dhidi ya timu ya Mzinga FC.

Mtenga alisema kuwa wana ndoto ya kutwaa ubingwa wa ligi daraja la tatu mkoa wa Morogoro na hilo linawezekana kutokana na kuwa na kikosi bora chenye wachezaji vijana na wenye vipaji vya kujua vyema mchezo wa soka.

“Wasichangae Shupavu FC kutwaa ubingwa wa ligi daraja la tatu mkoa wa Morogoro 2016/2017 kwani najua kila kocha anataka kutwaa ubingwa huu lakini wachezaji wangu wana kila dalili za kutwaa ubingwa huu.”alisema Mtenga.

Mtenga alifichua siri ya mikakati ya kuwinda taji hilo la ligi hiyo kuwa tangu waanze michezo ya hatua ya makundi hawajaweza kupoteza mchezo zaidi ya kutoa vipigo kwa kila timu ilikuwa inakutana nayo.

Hatua ya awali ya makundi katika kituo chetu katika ligi hii tulishinda mechi tatu na kutoa sare michezo miwili katika timu tano na hatua ya pili tukashinda michezo mitatu na sare mbili na kufanikiwa kutinga hatua ya sita bora.aliongeza Mtenga.

Mtenga alisema kuwa kwa sasa jopo la benchi la ufundi la Shupavu FC lipo katika mikakati kabambe ya kuandaa timu kwa michezo ya nusu fainali lakini malengo lao ni kutinga fainali na kutwaa ubingwa.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment