BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Millionaire  Ads

WANANCHI WAMKABA KOO MWENYEKITI WA MTAA ALIYETAFUNA FEDHA SH135,000 ZA KUANZISHA KIKUNDI MORO


Picha ya maktaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene akitoa ufafanuzi jambo hivi karibuni.

Juma Mtanda, Morogoro.
Morogoro.Afisa Mtendaji wa kata ya Uwanja wa Taifa ameombwa kuingilia kati ili kusaidia kurejeshwa kwa fedha Tsh. 135,000 za wananchi zinazodaiwa kukusanywa na Mwenyekiti wa mtaa wa Unguu B kwa lengo la kuunda kikundi cha wajasiriamali jambo ambalo hajalitekeleza. 


Akizungumza na MTANDA BLOG, mmoja wa wanakikundi, Rose Mbaga alisema kuwa Mwenyekiti wa Mtaa wao ametafuna fedha zao baada ya wananchi 45 kuchangishana Tsh3,000 kila mmoja tangu mwezi Machi lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea. 


Rose alisema kuwa walihamasishwa na viongozi wa kata hiyo kuunda vikundi vya usajiriamali ili iwe rahisi kukopeshwa fedha zilizoahidiwa na Rais Magufuli shilingi milioni 50 kwa kila kijiji. 


“Tunamwomba Afisa Mtendaji wa kata yetu aongee na Mwenyekiti wa Mtaa ili aweze kurejesha fedha zetu maana ameshindwa kuunda kikundi, kufungua akaunti benki wala kutayarisha katiba tangu mwezi wa tatu mwaka huu”alisema Rose. 


Kwa upande wa Mwenyekiti wa mtaa wa Unguu B, Benedict David alisema kuwa tuhuma zilizoelekezwa kwake juu ya kutafuna fedha kiasi cha sh135,000 sio za kweli isipokuwa mchakato wa kuunda kikundi upo katika hatua nzuri. 


David alisema kuwa kwa sasa tayari katiba ipo tayari imekamilika na suala la ufunguaji wa akaunti benki ni suala la wanakikundi wenyewe baada ya kupata viongozi. 


“Ni kweli nina fedha za wanakikundi 45 ambao kila mmoja alichanga kiasi cha Tsh3,000 lakini suala la mimi kula fedha zao sio la kweli isipokuwa ni wanakikundi wasiozidi 10 ndio wanataka kurejeshewa fedha zao na hao wengine wapo na mchakato wa kuendelea na kuunda kikundi,hao wanaohitaji fedha zao nitawarudishia”.alisema David. 


Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Uwanja wa Taifa, Omari Jaba alikiri kupokea malalamiko ya wananchi wa Mtaa wa Unguu B wakitaka kurejeshewa fedha zao ambazo zilikusanywa na Mwenyekiti. 


Omari alisema baada ya malalamiko hayo alimwita Mwenyekiti huyo na kumwagiza kuitisha mkutano wa wanakikundi hao ili kueleza kinachoendelea.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment
Millionaire  Ads