BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHRISTOPHER OLE SENDEKA WA CCM, ATEULIWA UKUU WA MKOA WA NJOMBE NA MAGUFULI


RAIS John Magufuli amefanya uteuzi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Mkoa. Rais pia pia amefanya mabadiliko katika wizara na mikoa. Profesa Faustin Kamuzora ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais. Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu Mawasiliano.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, iliyotolewa Dar es Salaam.

Taarifa hiyo ilieleza pia kuwa Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo.

Mhandisi Mtigumwe anachukua nafasi ya Dk Florens Turuka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kabla ya uteuzi huo, Dk Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi. Pia, Rais Magufuli amemteua Dk Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na atakuwa akishughulikia Mawasiliano.

Dk Sasabo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Kamuzora ambaye ameteuliwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Angelina Madete kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mhandisi Angelina Madete anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Maria Sasabo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano. Aidha, Rais Magufuli amemteua Dk Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Christopher Ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Sendeka anachukua nafasi ya Dk Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Dk Nchimbi anajaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Dk Osward Mashindano kuwa Msajili wa Hazina. Dk Mashindano anachukua nafasi ya Lawrence Mafuru ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: