Inaripotiwa kuwa mcheza mpira wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, na wachezaji wengine wa kandanda, wamekwepa kodi ya mapato yao ya mamilioni ya dola, kwa kupitisha fedha hizo kwenye njia za kuzighushi hadi nchi za ng'ambo kusikotozwa kodi.
Habari hizo zimechapishwa na gazeti moja la Ujerumani, Der Spiegel, na inasemekana zinatokana na data ya maelezo pamoja na kandarasi, makubaliano ya siri na barua pepe.
Mawakili wa Ronaldo wanasema, wakuu wa kodi wa Uspania wamekagua mapato yake na hawakuona kasoro yoyote. Jose Mourinho
Watu wengine maarufu wanaosemekana kutajwa katika ufichuzi huo, ni pamoja na Jose Mourinho, meneja wa Manchester United, ambaye kama Ronaldo, anawakilishwa na wakala Jorge Mendes.
Kampuni ya Bwana Mendes, Gestifute, inasema Mourinho amelipa kodi kamili kwa wakuu wa Uingereza na Uspania
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment