BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KASSIM MAJALIWA KUSHUGHULIKA NA ASKARI WANAOWATAWANYA WANANCHI KWA MABOMU YA MACHOZI MIGOGORO YA ARDHI

 
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amepiga marufuku Jeshi la Polisi nchini, kukodiwa na matajiri kwenda kunyanyasa wakulima kwa kupiga mabomu ili waachie ardhi kwa kisingizio ya uwekezaji.

Aidha amesema serikali kamwe haitakubali kuona wananchi wake wakinyanyaswa na kukosa ardhi wakati matajiri wachache wakiendelea kumiliki ardhi kubwa bila kuendeleza.

Majaliwa alitoa msimamo huo jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bwawani akiwa njiani kuelekea User River ambako alifanya mkutano mkubwa wa hadhara.

Waziri Mkuu alilazimika kupiga marufuku hiyo kutokana na wanakijiji hao kutoka kitongoji cha Omapinu kumshitakia kuwa wananyanyaswa na polisi wanaotumika na matajiri kuwaondoa kwa nguvu katika ardhi yao.


Wananchi hao wakiwa na zaidi mabango ya 20 yenye ujumbe tofauti ikiwamo ya ardhi, walielezea wanavyonyanyaswa na askari hao wanaotumiwa na matajiri ili kuwajenga hofu na kuwaondoa kwa nguvu katika maeneo yao kwa madai kuwa wameyavamia.

"Nimepata malalamiko mengi yanayohusu wananchi kupigwa kwa mabomu na baadhi ya kinamama kupoteza mimba zao kwa sababu ya kusulubiwa na polisi wanaotumwa na matajiri wanaodai kumiliki mashamba makubwa," alisema.

Majaliwa alisema kuanzia sasa ni marufuku kwa polisi kufanya hivyo na kusisitiza kuwa atakayetumiwa kunyanyasa wananchi atashughulikiwa. 


Waziri Mkuu alisema kutokana na kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji, atamtuma Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kifika wilayani Arumeru kushughulikia kero hizo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: