Klabu ya Polisi Moro SC inayojiandaa na michezo ya ligi daraja la kwanza Tanzania bara 2016/2017 mzunguko wa pili imeichalaza bila huruma timu ya soka ya Madale FC kwa kuitandika bao 2-0 katika ufunguzi wa ligi ya Morogoro Kwanza Bonanza 2016 katika mchezo uliofanyika uwanja wa Sabasaba mkoani hapa.
Mshambuliaji wa Polisi Moro SC, Juma Nade alianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 36 kwa shuti hafifu kufuatia krosi ya Abdallah Maidodi baada ya kumlamba chenga kipa wa Mandale FC na kukwamisha mpira huo kimiani.
Bao la pili na ushindi la Polisi Moro SC, lilifungwa na mshambuliaji, Gamba Iddi aliyetumia vyma pasi ya winga mshambuliaji wao tegemeo, Nicolaus Kabipe aliyewazidi mbio walinzi na kumimina majaro katika dakika ya 88 na kuzaa bao hilo la pili na ushindi.
Akizungumza na MTANDA BLOG kwenye uwanja wa Sabasaba mjini, Kocha Msaidizi wa klabu ya Polisi Moro SC, John Tamba alisema kuwa wameingiza kikosi kamili katika mashindano hayo kama sehemu ya mazoezi na maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza.
Tamba alisema kuwa Polisi Moro SC imeanza mazoezi rasmi (juzi) baada ya wachezaji kupewa likizo hivyo michezo hiyo wataitumia kukipima kikosi hicho na kurekebisha mapungufu.
“Mashindano haya yatatusaidia sana benchi letu la ufundi chini ya kocha mkuu, Ahmed Mumba kwa kurekebisha mapungufu ambayo yaliyojitokeza kwenye michezo ya ligi daraja la kwanza mzunguko wa kwanza ili mzunguko wa pili tufanye vizuri zaidi na kumaliza tukiwa vinara”alisema Tamba.
Unaweza kuona kuwa wachezaji walipewa likizo baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza uliomalizika kwa Polisi Moro SC kushika nafasi ya pili kwa pointi 14 mbele ya vinara wa kundi lao timu ya KMC FC yenye pointi 15 hivyo wanatumia michezo hiyo kama maandalizi tosha kuingia kwenye mapambano.aliongeza Tamba.
Mashindano hayo yanashirikisha jumla ya timu 16 na kuendeshwa katika mfumo wa mtoano ambapo timu inayoshinda inaingia moja kwa moja hatua ya robo fainali kisha nusu fainali na fainali.
Mshindi wa kwanza atazawadiwa pea 20 za viatu vya kuchezea soka wakati mshindi wa pili atakabidhiwa pea 15 za viatu huku mshindi wa tatu akiondoka na seti moja ya jesi na soksi na mshindi wa nne ataambulia seti moja ya jezi.
Timu zinazoshiriki ligi ya Morogoro Kwanza Bonanza 2016 ni pamoja na Kihonda Magholofani FC, Polista SC, Black People FC, Masubo FC, Chamwino Market FC, Gereji FC, Moro Kids FC na Obama FC.
Nyingine ni Kilakala FC, Chamwingo Rangers FC, Kaiza Chief FC, Beach Mzozo FC, Black Viba FC na Chicago FC.
0 comments:
Post a Comment