BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KLABU YA POLISI MORO YAELEKEZA AKILI NYINGI LIGI DARAJA LA KWANZA MZUNGUKO WA PILI

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Polisi Moro SC, Mahadh Bakari inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara akimiliki mpira dhidi ya, Kanedy Masumbuko wa timu ya Kagera Sugar wakati wa mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro ambapo Kagera Sugar ilishinda kwa bao 1-0.


Juma Mtanda,Morogoro.

Klabu ya Polisi Moro SC imeendelea kujiweka katika mikakati kabambe ya kuingia kwa nguvu kali kwenye mzunguko wa wa pili ligi daraja la kwanza Tanzania bara baada ya kufanya usajili na kujikita zaidi kucheza michezo ya kirafiki mkoani hapa.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Kocha mkuu wa klabu hiyo, Ahmed Mumba alisema kuwa timu hiyo kwa sasa inaendelea na mazoezi makali na kucheza michezo mingi ya kirafiki lengo benchi la ufundi kupata nafasi ya kufanyia kazi mapungufu yanayojitokeza na kufanyiwa kazi kabla ya kuingia mzunguko wa pili.

Mumba alisema kuwa Polisi Moro SC kwa sasa inahitaji kucheza mechi tatu na timu za ligi kuu Tanzania bara lakini mpaka sasa tayari wamecheza michezo miwili kati ya Simba SC na Kagera Sugar ambapo michezo hiyo walipoteza kwa kufungwa.

“Polisi Moro SC inahitaji michezo mitatu na timu za ligi kuu na tayari tumecheza michezo miwili dhidi ya Simba SC na tulifungwa bao 2-0 na Kagera Sugar nayo tukipoteza kwa bao 1-0 lakini leo (jana) tunajitupa tena uwanja kujipimana ubavu na Majimaji FC.”alisema Mumba.

Mumba alisema kuwa katika michezo hiyo benchi la ufundi itakuwa imejiridhisha kwa kukiona vyema kikosi chao ili kwenye mchezo wa kwanza mzunguko wa pili dhidi ya Coastal Union waweze kuibuka na ushindi desemba 17 kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro.

“Tumetengeneza safu nzuri ya umoja na mshikamano ndani ya timu kuanzia kwenye ushambuliaji, ulinzi na kiungo lakini kutokana na ingizo jipya la wachezaji tukiunganisha na wale wa zamani nina imani, Polisi Moro SC itakuwa moto wa kuotea mbali, kikubwa tuendeleze ushirikiano tu.”alisema Mumba.

Mpaka klabu hiyo imesajili baadhi ya wachezaji akiwemo kipa, Tony Kavishe (Mgambo JKT), Richard John na Godfrey Katabazi wote nafasi ya ulinzi kutoka klabu ya Mawenzi Market FC daraja la pili ya Morogoro.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: