Juma Mtanda, Morogoro.
Kikosi cha wachezaji wa klabu ya Simba SC kimetua mkoani Morogoro kwa ajili ya kuweka kambi ya kujianadaa katika michezo ya mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara.
Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Meneja wa timu hiyo, Mussa Hassan (Mgosi) alisema kuwa kikosi cha timu hiyo tayari kimetua katika ardhi ya Morogoro na kinatarajia kucheza michezo ya kirafiki kulingana na matakwa ya mwalimu, Joseph Omong.
Mgosi alisema kuwa, ijumaa wiki hii Simba SC itajipima nguvu na Polisi Moro SC inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara na michezo mingine itanyika kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi.
“Tumeingia Morogoro jana na kikosi kizima cha wachezaji wa klabu ya Simba SC lakini ijumaa wiki hii timu yetu itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Moro SC”.alisema Mgosi.
Simba inayoongoza ligi hiyo kwa kukusanya pointi 35 huku mabingwa watetezi Yanga SC ikishika nafasi ya pili ina pointi 33 wakati Toto Afrika FC ya Mwanza ikiburuza mkia kwa kuambulia pointi 12 ikifuatiwa na Mwadui FC ya Shinyanga yenye pointi 13 ikishika ya pili kutoka mkiani.
Katika maandalizi ya mzunguko wa kwanza, Simba SC iliweka kambi Morogoro na kucheza michezo kadhaa ya kirafiki ikiwemo na Polisi Moro SC ambapo katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa bao 6-0.
Katika mbio za kuwania taji hilo la ligi hiyo, Simba SC imeonekana kuweka hesabu zake katika njia moja baada ya upande safu ya ushambuliaji, Shija Kichuya akiibuka kinara kwenye mzunguko huo wa kwanza kwa kufumania nyavu akiwa na bao tisa huku vita hiyo ikiwa kali, Amis Tamwe wa Yanga akiwa na bao saba.
Wengine wenye bao saba ni pamoja na Rashid Mandawa, (Mtibwa Sugar), Simon Msuva (Yanga SC).
0 comments:
Post a Comment