BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAAJBU YA DUNIA, JE WAJUA NDEGE ANAYELALA HUKU AKIWA ANARUKA ANGANI ?.


Wanandi-pwani ni ndege wenye ustadi mkubwa wa kuruka angani na wamejaliwa kuwa na uwezo kuruka juu ya bahari kwa miezi kadhaa na kupumzika kwenye nchi kavu kwa siku chache tu lakini waporuka kwa miezi kadhaa, wanawezaje kulala?.


Watafiti wamechunguza wanandi-pwani jike 15 wanaoishi katika kisiwa cha Genovesa mashariki mwa bahari ya Pasifiki kwa siku 10.


Wakati mamalia na ndege wanapolala, mawimbi ya shughuli za ubongo huwa ni ya polepole huku watafiti wakigundua kuwa wanandi-pwani hao hawalali mchana, lakini saa moja baada ya jua kutua, mawimbi polepole ya shughuli za bongo zao yanaanza kutokea kwa mara chache. 


Hiyo inamaanisha kuwa ndege hao wanaruka huku wakiwa wamelala tena mawimbi hayo ya polepole yanapotokea, nyuso za ndege hao zinaelekea juu, kitendo ambacho hufanyika wanapolala katika nchi kavu.

 Wanandi-pwani wanalala katika hali mwafaka. Wanapoelekea juu kupitia upepo unaovuma juu wanalala, na wanaposhuka chini hawalali. 

Wanalala zaidi katika urefu mkubwa zaidi kutoka usawa wa bahari ambapo hatua hiyoi inapunguza uwezekano wa kuanguka baharini wanapokuwa na usingizi.

Aidha, wanandi-pwani wana uwezo wa kufanya nusu ya ubongo kupata usingizi na nusu nyingine kuendelea kufanya kazi. 


Uchunguzi unaonesha kuwa katika asilimia 70 ya muda wa kulala, wanalala kwa nusu ya ubongo tu. 
 
Katika asilimia nyingine 30, wanalala kikamilifu, lakini bado wanaweza kuruka vizuri.

Ingawa ndege hao wana ustadi wa kipekee wa kulala, lakini bado hawalali kwa muda mrefu wakati wanaporuka. Muda wa kulala unachukua asilimia 3 tu ya muda wote wa kuruka angani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: