BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA YA MATUKIO MOTOMOTO NDANI YA MKOA WA MOROGORO DESEMBA 10/2016.


Kaimu mratibu wa damu salama kituo kidogo cha Morogoro, Chiku James akimtoa damu, Nassoro Kisalala mkazi wa mtaa wa Madinizi kata ya Kilakala wakati mkazi huo alipotembelea kituo hicho katika jengo la msalaba mwekudnu kujitolea kutoa damu salama. PICHA ZOTE NA MTANDA BLOG.

Mhitimu wa shahada ya uzamili wa utawaka wa umma, Maliki Malupu akimpongeza, Santoangel Samike ambaye amehitimu shahada ya sayansi ya uchumi katika sera na mipango na kuibuka kidedea kwa kuwa mwanafunzi bora wa kike kitivo cha uchumi kwa kupata alama ya GPA 4.6 wakati wa mahafali ya chuo kikuu cha Mzumbe Morogoro, Malupu alikuwa mmoja wa wagombea nafasi ya urais katika kura za maoni ndani ya CCM katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.


Lori lililoharibika kisha kuegeshwa katika njia ya reli ya kati eneo la Ruaha mkoani Morogoro kwa kipindi kirefu kufuatia shirika la Reli Tanzania kusitisha safari ya Kilombero hadi Kilosa kutokana na sababu mbalimbali..


Kijana mkazi wa Manispaa ya Morogoro akiwa amebeba ndoo yenye vipande vya nanasi wakati akisaka wateja wake mtaa wa Ahamadiya ambapo kipande kimoja huuzwa kati ya sh100 hadi sh200 kulingana na ukubwa wake.

Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wakiangalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani baada ya kuhitimu elimu ya msingi na kubandikwa kwenye ukuta wa shule ya sekondari Morogoro.

Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa eneo la makutano ya mtaa wa Ahamadiya na Madaraka Manispaa ya Morogoro huku wakiwa wamepanga bidhaa ndogondogo chini wakati wakisubiri wateja wao, halmashauri ya Manispaa hiyo imepiga marufuku wafanyabiashara kuuza bidhaa katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood akizungumza jambo mara baada ya kukabidhi sehemu ya madawa na vifaa tiba vyemye thamani ya sh20.8mil kwa Msaidizi wa Mganga Mfawidhi kituo cha afya Manispaa, Mhinah Mwagilo wa pili yake na diwani wa kata ya Mafiga, Spear Komanya wa kwanza kushoto wakati wa tukio hilo.

Mkaguzi wa jeshi la Polisi, Masala Mugema akihakiki pikipiki baada ya kufanya operesheni ya ukamataji salama na utoaji elimu juu ya usalama barabarani kwa vyombo vya motokwa madereva wa pikipiki Manispaa ya Morogoro ikihusisha makosa ya kutovaa kofia nguvu (Elment) na mengine katika eneo la shule ya Msamvu barabara kuu ya kuingia Mjini.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: