BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Mashamba yachomwa mara 16, vyombo vya dola vyaamshwa


VYOMBO vya ulinzi na usalama vimetakiwa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio ya mashamba ya miwa ya kiwanda cha sukari kuchomwa moto mara 16 na watu wasiojulikana na kusababisha hasara ya Sh. bilioni 9.7 visiwani hapa.

Mwakilishi wa Mpendae Mohamed Said, alitoa pendekezo hilo katika Baraza la Wawakilishi jana wakati akiwasilisha hoja binafsi kuhusu matukio hatarishi katika sekta ya uwekezaji wa viwanda Zanzibar.

Alisema mashamba ya miwa ya wawekezaji wa kiwanda cha sukari yamekua yakichomwa moto mara kwa mara na kusababisha hasara kubwa kwa wawekezaji hao, lakini hakuna muhusika yeyote aliyekamatwa hadi sasa.

“Kuna vitendo mbalimbali vinafanywa kwa makusudi ndani ya Zanzibar ambavyo vinahatarisha uwekezaji wa viwanda.”
"Wawekezaji wanaotaka kuwekeza huangalia mambo mbalimbali, ikiwamo sera za uwekezaji, usalama na mambo mbalimbali yanhayojitokeza katika nchi kabla ya kuanza uwekezaji," alisema.

Mwakilishi huyo alisema kuanzia Aprili 16, mwaka 2015, mpaka Machi 8, mwaka huu, matukio 16 ya mashamba kuchomwa moto yamefanyika na kusababisha hasara ya Sh. bilioni 9.7 na wafanyakazi kuwa katika hatari ya kupoteza ajira.

“Serikali kupitia vikosi vyake vya ulinzi na usalama na kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) ifanye upelelezi wa kutosha ili kubaini chanzo cha mashamba ya miwa kuhujumiwa na wahusika ni nani,”alisema.

Mohamed alipendekeza serikali ya mkoa wa Kaskazini kupitia kamati ya ulinzi na usalama iweke mikakati madhubuti ili kuimarisha ulinzi katika mkoa huo hasa katika maeneo ya uwekezaji.

Aidha, alipendekeza itolewe elimu ya ulinzi shirikishi baina ya vikosi vya ulinzi na usalama, Jeshi la Polisi na wananchi ili waelewe umuhimu wa kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao na nchi kwa ujumla.

Alisema viongozi wa serikali za mitaa (masheha) watoe ushirikiano wa kutosha kwa vikosi vya ulinzi na polisi ikiwamo kutoa taarifa za watu wanaohusika na vitendo hivyo kwa manufaa ya Zanzibar na wananchi wake.

Alisema amewasilisha hoja binafsi kwa kutumia kanuni ya 2791) (n) 27 (1) na 50 ya Baraza la Wawakilishi ili kulinda sekta ya uwekezaji wa viwanda visiwani hapa.

Wajumbe waliochangia hoja hiyo ni Ali Suleiman Ali (Kijitoupele), Simai Mohamed Said (Tunguu) na Hamza Hassan Juma (Shaurimoyo), ambao walitaka serikali kufanya uamuzi mgumu ili kukomesha vitendo vya wanaofanya hujuma hizo na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa maslahi ya Zanzibar na wananchi wake.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: