BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBU WA MALARIA WAJENGEWA KIWANDA TANZANIA


KIWANDA cha kuzalisha bidhaa za kibailojia, zikiwemo viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu waenezao malaria na mbolea kimeanza uzalishaji miezi miwili sasa.

Ofisa Mauzo kutoka Kampuni tanzu ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), ijulikanayo kama Tanzania Biotech Products Ltd, Frank Mzindakaya alisema jana jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa bidhaa hizo huzalishwa kwa kutumia teknolojia toka Cuba.

Mzindakaya alisema kwa sasa kiwanda hicho kinazalisha dawa za aina mbili ambazo ni ‘Bactivec na Griselesf’ zinazotumika kunyunyuzia kwenye mazalia ya mbu. Alisema dawa hizo zinatumika kwa kumwagiliwa kwenye madimbwi ya maji yaliyotuwama ambayo ni mazalia ya mbu.

“Zikishatumika kwenye madimbwi ya maji yaliyotuama, dawa hiyo huvutia viluwiluwi na kula kama chakula ambayo hugeuka kuwa sumu,” alisema Mzindakaya.

Alisema hapa nchini wateja wao wakubwa ni Halmashauri zote ambazo baadhi yao katika mkoa wa Dar es Salaam wameshafanya mazungumzo, pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Pia kwa sasa wanaandaa oda kwenda nchini Niger.

Alitoa wito kwa watanzania wote kutoa ushirikiano kwa waratibu wa malaria ili kuweza kutambua vyanzo vya mazalia ya mbu ikiwa ni pamoja na kutumia dawa hizo kuondokana na tatizo la malaria nchini.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: