MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameagizwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuendelea kuchunguza gharama za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Monduli iliyojengwa kwa fedha nyingi za serikali.
Hospitali hiyo ambayo imejengwa kwa fedha za serikali kwa gharama ya Sh bilioni 2.7 ambapo haina jengo la upasuaji karibu na wodi ya wazazi pamoja na maabara.
Waziri Mkuu alisema hospitali hiyo itasaidia kutatua changamoto za afya kwa wananchi, lakini alishangaa ni kwa nini gharama za ujenzi huo kuwa kubwa na kumwagiza Gambo kuendelea na uchunguzi juu ya fedha hizo ili kujua kama kweli fedha hizo zilitumika kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo au la.
“RC endelea na uchunguzi wa fedha hizi za serikali wewe na timu yako uliyoiunda ili kubaini je, ni kweli fedha hizi zimetumika kujenga hospitali hii au la maana gharama za ujenzi ni kubwa kuliko uhalisia wa hospitali hii,” alisema.
Aliagiza wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaoza watoto wa kike, kwani serikali ikibaini kuwa kuna mzazi au mlezi kaoza mtoto wake au kashiriki kupeleka posa atachukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwemo kifungo cha miaka 30 jela.
Awali Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Zaveri Benela akisoma taarifa ya hospitali hiyo, alisema licha ya kujengwa majengo hayo na serikali kutoa fedha, lakini inakabiliwa na ukosefu wa jengo la upasuaji karibu na wodi ya wazazi kwani bado wanasafirisha wagonjwa kwa zaidi ya mita 300 hadi kwenye jengo la upasuaji kwenye majengo ya zamani.
Pia kukosekana kwa jengo la wagonjwa wa nje na jengo la maabara kwenye majengo hayo, hali inayosababisha huduma hiyo kutolewa kwenye maeneo miwili tofauti kwa wakati mmoja yaani wodi mpya na majengo ya zamani na hali hiyo inaleta usumbufu kwa wagonjwa.
Alisisitiza kuwa ujenzi wa jengo la upasuaji na jengo la wagonjwa wa nje ulikuwepo kwenye awamu ya pili wa ujenzi wa hospitali hiyo mpya ambapo halmashauri iliomba fedha mwaka jana bila mafanikio.
Alisema wilaya hiyo ya Monduli ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 41, zahanati 37, vituo vya afya vitatu na hospitali moja ya wilaya, lakini bado wana upungufu wa watumishi wa afya 391 katika kada mbalimbali.
Ujenzi huo mpya wa hospitali ya wilaya ulianza Machi, 2013 kwa makandarasi wawili kupewa kazi ya ujenzi wa majengo hayo na mkandarasi wa kwanza ni Meero Contractors aliyepewa Block A kwa jumla ya Sh 1,482,993,072.20 na mkandarasi wa pili Bullem Investment alipewa Block B kwa jumla ya Sh 1,438,683,300.00.
Alisema majengo hayo miwili yana jumla ya wodi nne zenyewe vitanda 128, vyumba vya kujifungulia vitatu, vyumba vya watoto wachanga na wanaozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) viwili.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment