BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTANGAZAJI WENYE SAUTI YA KUMTOA NYOKA PANGONI KAREE OMAR ATUA SWAHILI FM 93.1 MOROGORO.


Mtangazaji maarufu hapa nchini, Kareem Omar a.k.a KO ama ukipenda unaweza kumwita Shulekongwa ameanza kufanya kazi katika kituo cha kipya kinachorusha matangazo yake vizuri mkoani Morogoro na mikoa ya jirani cha SWAHILI FM 93.1.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Kareem alieleza kuwa kituo hicho kinarusha matangazo yake jengo la NSSF mkabala na ofisi za Manispaa ya Morogoro akihusika kikamilifu kutangaza kipindi cha LOUDSPIKA kwa siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia majira ya saa 7 mchana mpaka saa 10 alasiri kwa burudani ya muziki na habari motomoto zinazowahusu wanamuziki na muziki.

Kipindi hicho kinaendana na kutoa maoni kwa njia ya ujumbe mfupi (sms) kupitia namba 0621009580 lakini unaweza kumpata kwa kumfollow instra dj_ko_shulekongwe huku mtandao wa fesibuku akipatikana na anuani ya kareem omar ko wakati upande wa barua pepe anapatikana kwa anuani ya shulekongwe1@gmail.com.

Kituo hicho cha SWAHILI FM 93.1 kina na kaulimbiu ya LUGHA YETU SAUTI YETU.


Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: