BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI AIBUA MJADALA NAFASI YA GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA PROF NDULU

Kuenguliwa kwa Lawrence Mafuru kutoka nafasi ya Msajili wa Hazina, kumeibua mjadala wa nafasi ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu, ambaye alikuwamo kwenye Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo Rais aliivunja mwezi uliopita.

Kuondolewa kwa Mafuru na nafasi yake kujazwa na Dk Oswald Mashindano, kunaweza kuwa ni moja ya muendelezo wa harakati za Rais John Magufuli kutengeneza timu yake ambayo anaamini itaendana na kasi yake.

Mafuru, ambaye aliteuliwa kushika nafasi hiyo mwaka 2014, aliondolewa siku chache baada ya kutoa kauli iliyoonekana kutofautiana na ya Rais kuhusu suala la wakurugenzi wa taasisi za umma kuweka fedha kwenye akaunti za muda maalumu na baadaye kuchukua ongezeko linalotokana na riba, kwa ajili ya matumizi yao binafsi.

Wakati Rais akisema wakurugenzi wakuu wa taasisi za Serikali huweka fedha kwenye akaunti hizo maalumu na baadaye kujinufaisha na riba, Mafuru alisema haiwezekani watumishi hao kuchota fedha za umma kutoka benki kwa kuwa miamala ni ya wazi na akaongeza kuwa wamemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuzikagua.

Kauli yake ilikuja siku mbili baada ya Gavana Ndulu kutoa kauli kama hiyo akiwa mjini Arusha, aliposema kuwa hakuna sheria inayozuia taasisi za Serikali kuweka fedha kwenye akaunti ya muda maalumu, ambazo riba yake huzalisha faida ambayo Rais Magufuli alisema imekuwa ikichotwa na kutumiwa kwa masilahi kwa binafsi na viongozi wa taasisi hizo.

Mjadala huo usio rasmi uliibuka baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi ya TRA, Bernard Mchomvu Novemba 20 na kutangaza kuivunja bodi yote.

Siku nne baadaye, Rais alisema alichukua uamuzi huo baada ya bodi kuidhinisha maombi ya TRA ya kuweka fedha kwenye akaunti ya muda maalumu.

“Juzi hapa tumekuta Sh26 bilioni zilizokuwa zimetolewa TRA kwa ajili ya matumizi ya TRA, zikapelekwa kwenye mabenki matatu kama ‘fixed deposit account’ na bodi ikapitisha. Ndiyo maana nilipozipata hizo hela, nikazichukua na bodi kwaheri,” alisema Rais Magufuli alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 31 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Tangu wakati huo, Rais hajatangaza hatua zozote dhidi ya wajumbe wa bodi hiyo, ambao watano kati yao wanaingia kutokana na nyadhifa zao. Wajumbe hao ni Gavana wa BoT, Kamishna Mkuu wa TRA, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar na Katibu Mkuu wa Mipango.

Lakini kati yao, ni Gavana Ndulu pekee aliyejitokeza kuzungumzia suala hilo, na kauli yake—kama ilivyokuwa ya Mafuru—inaonekana kutofautiana na Rais Magufuli.

“Kwani (Rais) amesema fixed account zote ni mbaya pamoja na za watu binafsi? Ndiyo hivyo sasa. Nilijua mtachomekea hilo kwa hiyo nilikuwa tayari,” alisema mhadhiri huyo wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati alipozungumza na waandishi mjini Arusha alikoenda kuhudhuria mkutano wa taasisi za fedha. Wadadisi wanasema hiyo inaweza kuwa sababu kubwa ya Rais kufanya mabadiliko kwenye nafasi hiyo.

Sababu ya pili inayoweka rehani nafasi ya Gavana Ndulu ni ukweli kwamba alikuwa mjumbe wa bodi ambayo iliidhinisha fedha kuwekwa kwenye akaunti ya muda maalumu baada ya Rais kutoa maagizo ya kuzuia fedha za umma kuwekwa kwenye akaunti hizo.

Ukiacha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha - Zanzibar, wateule wengine watatu—Kamishna Mkuu wa TRA, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha (Muungano) na Katibu Mkuu wa Tume ya Mipango—ni wateule wapya na huenda bado ana imani nao.

Sababu nyingine ambayo si muhimu sana lakini inayoweza kuwa na maana kipindi hiki, ni ukweli kwamba Rais anapanga safu yake ya uongozi, hasa katika taasisi nyeti.

Ndulu amekuwa kwenye nafasi hiyo tangu mwaka 2008 baada ya aliyekuwa Gavana, Daudi Balali kuenguliwa kutokana na sakata la malipo ya fedha kwa wafanyabiashara kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa).

Baada ya kufanya kazi na Gavana Ndulu kwa mwaka mmoja, sasa Rais Magufuli anaweza kufanya mabadiliko ya mkuu wa taasisi hiyo nyeti bila ya kuweka hofu kwa jumuiya ya wahisani, wafanyabiashara na wawekezaji, ambao uamuzi wao kuhusu masuala ya kifedha hutegemea uimara wa chombo hicho.

Wachambuzi wazungumza Profesa wa Uchumi katika Kilimo wa Chuo Kikuu cha Sokoine (Sua), Damian Gabagambi alisema kwa sababu Rais hakusema sababu za kutengua uteuzi wa Msajili wa Hazina, inawezekana zipo nzuri na tofauti kabisa.

Alisema kama sababu ni kuhusu kupishana kwa kauli zao kama ilivyokuwa kwa Mafuru, basi na nafasi ya Gavana itakuwa shakani kwa sababu na yeye alifanya jambo kama hilo.

Alisema pamoja na mambo yote, bado ipo haja ya kufikiria mara mbili kuhusu Gavana kwa sababu yupo katika nafasi nyeti na inayohitaji umakini na kuaminika zaidi.

“Kama kweli sababu zinazodhaniwa, ambazo mimi binafsi hainiingii akilini kuwa nchi imefika hapa ilipo zikiwa kweli, basi hakutakuwa na maoni ya kitaalamu badala yake watu watatoa kulingana na Rais anataka kusikia nini.

“Kwa utaratibu huo nchi itakuwa na wanafiki badala ya watendaji wanaofanya kazi, kutoa maoni kitaalamu, tutafurahi kwa muda mchache, lakini baada ya muda tutagota,” alisema Profesa Gabagambi.

Naye Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Ruco)

alisema kama sababu zilizomuondoa mtu makini kama Mafuru ni hizo litakuwa siyo jambo zuri kwa maendeleo ya nchi.

“Kama sababu ni hiyo, ina maana wale wote waliopingana na Rais katika kutoa maelezo ya kitaalamu wajiandae akiwamo Gavana, ingawa kuna ukakasi kukubali na kuamini kuwa mtu anayejibu kitaalamu anaonekana mbaya sababu tu watu wanataka kusifi alisema.

“Kama hivyo ndivyo, hali ita mbaya zaidi huko baadaye na ha mtaalamu atakayetoa maoni hata yatakapohitajika kwa mustakaba Taifa, ”alisema Profesa Mpangala Gavana Ndulu alipoulizwa ku suala hilo alijibu kwa kifupi, “siyo Ikulu siwezi kulizungumzia kwa heri”.

Wadau wamzungumzia Mafuru Kwingineko, wasomi na wana wamedodosa mabadiliko yaliyofa na Rais, wakitaka madaraka yake galiwe upya katika Katiba Mpya.

Mafuru aliondolewa katika n hiyo wakati Rais alipotangaza ma liko ya watendaji katika serikali ambako aliyekuwa msemaji wa Christopher Ole Sendeka anaye Mkuu wa Mkoa wa Njombe, uteu balozi mmoja na mabadiliko ya m tibu wakuu wa wizara.

Akizungumzia mabadiliko hayo fesa Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chang’ombe (Duce), alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano inampa mamlaka makubwa Rais.

“Huo ni mtindo wake wa uongozi na Katiba ya Jamhuri inampa madaraka hayo. Swali ni kwamba madaraka hayo ni sahihi? Anaweza kuteua na kutengua wakati wowote bila kushauriana na yeyote? Hii ndiyo sababu ya wananchi kutaka mabadiliko ya Katiba kwa sababu inamfanya kuwa kama mungu wa pili,” alisema.

“Anachokifanya Rais Magufuli ni ushahidi wa kile tulichokuwa tunakisema kinadharia kuhusu madaraka makubwa aliyonayo Rais. Anatusaidia kutuonyesha ubovu wa Katiba yetu na sababu ya kutaka mabadiliko.”

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, Julius Mtatiro alisema mabadiliko hayo ni staili yake na kwamba itaendelea hadi 2020.

“Ukichunguza hizi sekta na taasisi anazohamisha watendaji wake hazipigi hatua. Hali hii inasababisha kusiwe na taasisi imara,” alisema Mtatiro.

Mtatiro alisema inaonyesha kama Rais amelipiza kisasi kwa mtaalamu aliyetoa maoni yake hadharani yaliyokwenda tofauti na alichokisema yeye.

“Hii ni sms (ujumbe) kwa watendaji watakaokwenda kinyume na kwa kila jambo analoliamini Rais Magufuli.

Mafuru alisimama katika ukweli kutokana na profession (utaalamu) yake,” alisema.

Mjumbe wa Jukwaa la Katiba, Hebron Mwakagenda alisema Katiba za nchi nyingi zinatoa madaraka kwa marais kuteua na kutengua viongozi na watendaji wa Serikali bila kushauriwa na mtu.

“Sina tatizo na hilo, ila kwa watumishi wa umma, anapaswa kuangalia. Tumekuwa tukisikia watu wakitenguliwa na kuambiwa watapangiwa kazi nyingine, lakini hadi leo hawajapangiwa. Akiteua mkurugenzi mwingine wanakuwa wawili, ila mmoja anafanya kazi, kwa hiyo hapo kubana matumizi hakupo tena,” alisema.

Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Juju Danda alisema hakubaliani na uamuzi huo wa Rais kumuondoa Mafuru kwa kuwa hakulenga kumkosoa Rais.

“Ifike mahali Rais aweke utaratibu wa kuamini watendaji wake. Sikuona kosa la Mafuru... ni mtaalamu na alikwenda kufafanua hoja,” alisema Danda.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu alisema suala la panga pangua si jambo baya na geni kwa Rais Magufuli ila sababu zinaweza zikawa shida.

“Leo hii ukiniuliza Rais Magufuli katika panga pangua yake amelenga nini sijui? Kwa sababu yupo katika kila sekta na kazi zote anazifanya yeye,” alisema Mwalimu. Alisema haoni tatizo la akaunti za muda maalumu na kwamba Mafuru alieleza vizuri na si kisiasa kwa kuwa ni mtaalamu. “Sina uhakika kama ni sababu ya kueleza ukweli ndiko kumemponza au la? Kama zipo sababu Rais atueleze,” alisema.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: