BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA SC YAJIWINDA KIVINGINE MZUNGUKO WA PILI LIGI KUU TANZANIA BARA

Mshambuliaji wa Simba SC, Jamal Mnyate akiwa katika hekaheka za kumiliki mpira huku mlinzi wa Polisi Moro SC, Jonathan Mujaibindi akiwania mpira huo wakati wa mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu baina ya timu hizo kwenye uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro ambapo Polisi Moro SC ililala kwa bao 2-0.PICHA/MTANDA BLOG

Juma Mtanda, Morogoro.
Klabu ya Simba SC inayojinoa kwa ajili ya kujiimarisha katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara mzunguko wa pili, baada ya kuilaza Polisi Moro SC kwa mbinde na kuibuka na ushindi bao 2-0 wakati wa mchezo mkali wa kirafiki wa kujipima nguvu uliopigwa kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro.

Wekundu hao wa Msimbazi wanaoongoza ligi hiyo kwa pointi 35 huku mabingwa watetezi klabu ya Yanga SC ikiwanyemelea kwa kushika nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi 33 ambapo Simba imeweka kambi mkoani Morogoro.

Simba SC walilazimika kusubiri hadi dakika ya 66 kupata bao la kuongoza baada ya mshambuliaji, Ibrahim Ajibu kufunga bao kwa tiktaka kufuatia krosi iliyochongwa na Bukungu Besala kutemwa na kipa wa Polisi Moro SC, Benjamin Haule na kujaza mpira huo kimiani.

Bao la pili la Simba lilikwamishwa wavuni na Abdi Banda dakika ya 75 akiunganisha vyema mpira wa kona uliomiminwa na mlinzi huyo, Bukungu Besala na kuandika bao la pili na ushindi katika mchezo huo.

Benchi la ufundi la Simba iliwachezesha wachezaji wake wawili waliosajiliwa katika dirisha dogo huku kipa mpya, Daniele Agrey akicheza dakika 90 tofauti na Jemsi Kotey aliyeingia kipindi cha pili na kucheza dakika chache.

Mabadiliko yaliyofanywa na Simba kipindi cha pili cha kumtoa, Jamal Mnyate na kuingia, Ibrahim Ajibu kuliongezea uhai safu ya ushambuliaji iliyokuwa ikiongozwa na Leydit Mavugo, Shija Kichuya, Federic Blaginon, Yassin Mzamiru na Said Ndemla ambao walishindwa kuelewana.

Nafasi zao zilichukuliwa na Mussa Ndusha, Jonas Mkude, Mohamed Ibrahim, Ugando Hija na Jemsi Kotey.

Kipindi cha kwanza Simba walitengeneza mashambulizi mengi lakini safu ya ulinzi wa Polisi Moro SC ilikuwa imara na kuondosha hatari zote zilizokuwa zikielekezwa langoni mwao huku kipa Benjamin Haule akionekana kikwazo kwa washambuliaji wa Simba.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja alisema kuwa mchezo huo ulikuwa mzuri kwa timu yake na suala la kupata ushindi halikuwa la umuhimu bali ni kuangalia ushirikaino wa wachezaji baada ya kutoka kwenye mapumziko wa mzungo wa kwanza ligi kuu Tanzania bara.

Mayanja alisema kuwa mashabiki na wadau wa klabu ya Simba wamechoshwa na kitendo cha klabu hiyo kushindwa kutwaa ubingwa kwa misimu minne mfululizo jambo linalowasononesha na kukosa furaha kutokana na matokeo ya misimu iliyopita.

“Benchi la ufundi la Simba lina thamira moja tu ya kuhakikisha Simba msimu huu inatwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara ndio maana tunafanya kila tunaloweza kufanya timu ipate matokeo na ikitokea tumekosa ubingwa hayo sio malengo yetu”alisema Mayanja.

Mayanja alisema kuwa katika kujiimarisha kila idara, ndio maana kipa wao mpya, Daniel Agrey alianzishwa kwenye mchezo dhidi ya Polisi Moro SC ili benchi kuona uwezo wake katika mchezo huo dhidi ya timu ya Polisi Moro SC inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

“Huwezi kumwangalia mchezaji kwenye michezo ya ushindini, tumeona Polisi Moro SC ni ndogo hivyon ni nafasi mzuri ya kuangalia wachezi na tumeona Jemsi Kotey aliingia kipindi cha pili na tunaendelea kuisuka hii timu ili iendelee kuwa kali zaidi mzunguko wa pili.”alisema Mayanja.

Kwa upande wa kocha wa Polisi Moro SC, Ahmed Mumba alisema kuwa mchezo huo ulikuwa mzuri licha ya poteza kwa bao 2-0.

Tumepoteza mchezo huu lakini haikuwa malengo yetu kupoteza bali nasi tumetumia kuangalia wachezaji wetu wapya tuliowasajili dirisha dogo na lengo mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza kufanya vizuri kutoka nafasi ya pili na kukaa nafasi ya kwanza.aliongeza.

Polisi Moro SC yenye pointi 14 mbele ya vinara wa kundi lao timu ya KMC FC ya Temeke jijini Dar es Salaam wakidhamilia kuipiku nafasi hiyo na kuwa vinara wa kundi lao ili kurejea ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.

Simba kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara msimu huu iliweka kambi Morogoro ambapo katika mchezo wa kujipima nguvu na Polisi Moro SC ilifanikiwa kuinyima kwa bao 6-0 huku ikipata ushindi wa bao 4-0 mbele ya Burkina FC iliyopo daraja la pili na kuambulia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa KMC Fc iliyopo ligi daraja la kwanza.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: