BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAANDISHI WALIOMWANDIKA VIBAYA MZEE WA UPAKO WATAKUFA KABLA YA MWEZI WA TATU 2017


Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo.


Maarufu Mzee wa Upako Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu Mzee wa Upako amesema waandishi wote wanaoandika habari za kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.

Kauli hiyo aliitoa jana ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yaliyoandikwa kwenye vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa.

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mpo humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: