Nahodha wa timu ya sokaa ya Taswa FC Morogoro, Nickson Mkilanya ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa huo (MoroPc)
Juma Mtanda, Morogoro.
Kikosi cha timu ya soka cha Kupamba na Ujambazi FC katika jeshi la polisi mkoa wa Morogoro kipo katika maandalizi makali ya kujiandaa kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya timu za Taswa FC na tiGO FC mkoani hapa.
Michezo hiyo ina lengo la kuendeleza na kudumisha mahusiano kati ya vyombo vya habari na makampuni ya simu za mkononi kutoakana na namna wanavyoshirikiana katika utendaji kazi wa kila siku katika ofisi hizo.
Kabla ya kuanza kwa michezo hiyo, viongozi wa jeshi la polisi watatoa elimu juu ya namna nzuri ya kutoa taarifa za matukio ya kiuharifu huku jeshi hilo likiwa tayari kupokea changamoto na kero mbalimbali kutoka kwa wadau, kisha kufanyiwa kazi ili raia waendelee kuishi maisha yenye amani na usalama.
Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Nahodha wa kikosi hicho, Hamis Mnunguye alisema kuwa kikosi chao kipo katika maandalizi makali ya ajili kucheza michezo hiyo itayofanyika kwenye uwanja wa jamhuri mkoani haoa.
Mnunguye alisema kuwa Desemba 4 siku ya jumapili mwezi huu, kikosi chake kitashuka dimbani kutandaza soka la kiwango cha juu mbele ya vijana wa timu ya tiGO fc saa 2 asubuhi kwenye jamhuri kisha kufuatiwa na mchezo na timu machachali ya soka ya waandishi wa habari za michezo mkoa wa Morogoro (Taswa FC).
“Lengo la michezo hii ni kucheza soka pamoja na waandishi wa habari na wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya tiGO ili kuweza kubadilishana mawazo na kupeana mbinu za kuendeleza ushirikiano ili kuwafichua waharifu ndani ya jamii zetu.”alisema Mnunguye.
Mnunguye alisema kuwa michezo ina faida kubwa ikiwemo kujenga afya lakini kwa jeshi la polisi, waandishi wa habari na makampuni ya simu za mkononi vyombo.
Vyombo vya habari (Waandishi) wamekuwa na mchango wa kutoa taarifa kwa jamii zinazotoka ndani ya jeshi la polisi huku makampuni ya simu yakisaidia jeshi kukabiliana na wahalifu kwa njia ya mitandao.
Kwa upande wa nahodha wa timu ya soka ya Taswa FC, Nickson Mkilanya alisema kuwa kikosi chao kwa sasa hakina mazoezi ya kufanya kuwezesha kucheza mchezo wa ushindini hivyo wanahitaji kuiandaa timu ili waweze kuvaana nao.
Taswa FC Morogoro ina kikosi kizuri kinachotokana na kusheheni wachezaji wenye vipaji vya soka kama Peter Kimath, Halfan Diyu, McNamara Nghambi, Abeid Dogoli, Kuty Libenga, Samuel Msuya, Daud Juliani na wengine wengi kibao.alisema Mkilanya
Mkilanya alijigamba kwa kusema kuwa hicho kikosi cha soka cha Kupambana na Ujambazi FC, wajiandae kisaikolojia kwani Waandishi wamedhamilia kuwafundisha soka linavyochezwa lakini lazima wafungwe idadi kubwa ya mabao.
“Tuna taarifa za mwaliko wa kucheza mchezo wa soka na kikosi cha timu ya soka ya kupambana na ujambazi FC lakini kwa sasa hatuwezi kucheza mchezo wowote wa ushindani kutokana na waandishi kukabiliana na majukumu ya utendaji wa kazi za kila siku na kukosa muda wa kufanya mazoezi”alisema Mkilanya.
Mkilanya aliongeza kwa kusema kuwa ni jambo zuri kwa taasisi ya jeshi la polisi kuandaa michezo, kwani inasaidia kuwa karibu na wadau ndani ya jamii, nina imani itasaidia polisi kupata taarifu nyingi za kiharibu kutoka kwa raia wema.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment