BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HABARI MPYA !!! WATU 15 WALIOFUKIWA NA KIFUSI KATIKA MGODI WOTE WAOKOLEWA GEITA

 
Baadhi ya watu 15 wakiwa wamelala chini mara baada ya kuokolewa kutoka chini ya ardhi katika mgodi wa dhahabu wa RZ Union mkoani Geita kufuatia kukwama tangu juzi kwa kifusi kuziba njia ya kutokea na kushindwa kutoka nje.

Katika zoezi hilo imeelezwa kuwa waokoaji katika mgodi huo walikuwa wamebakiza mita tatu kuwafikia katika juhudi za jana za kuwaokoa na hatimaye leo zoezi hilo limefanikiwa kwa 100% kwa  wachimbaji wote 15 kuokolewa akiwemo raia mmoja wa kigeni kutoka China.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani alieleza tukio hilo namna linavyoendelea.


Jana walifanikiwa kufanya mawasiliano na wachimbaji hao na kujeresha ujumbe kuwa wapo 15, ujumbe uliotumwa na waokoaji kwa njia ya kamba na kalamu kisha kuwafikia na kurejesha majibu.alisema Naibu Waziri.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment