BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Millionaire  Ads

MADEREVA WA DALADALA WAFANYA MGOMO ZAIDI YA SAA 5 MOROGORO


Juma Mtanda, Morogoro.
Madereva wa daladala Manispaa ya Morogoro wameendesha mgomo wa kutoa huduma ya kusafirisha abiria kwa muda wa zaidi ya saa 5 na kusababisha kero na usumbufu katika barabara kuu ya Dodoma-Morogoro eneo la Msamvu mkoani hapa.

Mgomo huo ulianza majira ya saa 12 asubuhi jana kwa daladala za Kihonda-Mjini kukusanyika kituo cha daladala cha ndani ya stendi ya mabasi yaendayo mikoani Msamvu wakati wakigomea kulipa ushuru wa Sh3000 kwa kutwa katika stendi tatu tofauti.

Kutokana na mgomo huo, daladala ziliziba barabara kuu ya kuingia stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ya Msamvu na kushindwa kutumia lango hilo na kulazimika kutumia mlango mwingine kuingia katika stendi hiyo.

Wakati mgomo huo ukiendelea, madereva na makondakta wao waliendesha zoezi la kushusha abiria waliokuwa wanasafirishwa kupitia pickup ama daladala hali iliyosababisha usafiri eneo la Msamvu kuwa mgumu na kulazimika wasafiri kukodi pikipiki ili kuendelea na safari zao.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Mmoja wa madereva hao, Omari Mahimbi alisema kuwa mgomo huo umetokea baada ya madereva kupinga kulipa ushuru wa Sh1,000 wa stendi ya daladala ya Msamvu unaomfanya dereva mmoja kwa siku kulipa ushuru kiasi cha Sh3,000.

Mahimbi alisema kuwa kuwepo kwa ushuru wa Sh1000 katika stendi ya daladala Msamvu kunamfanya dereva kulipa kiasi cha Sh3000 kwa siku huku kwa mwezi akilipa kiasi cha Sh90,000 jambo wanalodai linawaumiza na kushindwa kufanya maendeleo katika familia zao.

“Hebu fikiria stendi tatu ndani ya Manispaa moja zinatulazimu tulipe sh3000 kwa siku kwa stendi ya Masika, Msamvu na mjini na dereva anajikuta analipa ushuri wa Sh90,000 kwa mweizi kiwango ambacho ni kikubwa tofauti na kipato tunachopata kwa siku.”alisema Mahimbi.

Mgomo huo umehusisha daladala zinazotoa huduma kwa kusafirisha abiria kati ya Kihonda na mjini pekee.

Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood aliyewasiri majira ya saa 2:15 asubuhi katika eneo la Msamvu alisikiliza matatizo ya madereva hao na kuagizwa kuwaita mkuu wa wilaya na mkurugenzi ili wasikilize kilio chao eneo la tukio.

“Nimefika hapa saa 2:15 na nimesikiliza matatizo yao lakini wamenitaka niwaitie Mkurugenzi na DC ili madereva hawa wapate nafasi ya kusikizwa kero zao zinazosababisha wao kufanya mgomo huu na bahati nzuri DC wetu, Regina Chonjo amefika na tumeyapatia ufumbuzi matatizo yao.”alisema Abood wakati akiongea na waandishi wa habari.

Akizungumza na madereva hao, Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo alisema kuwa ushuru wa stendi ya daladala Masika umesitishwa na stendi ya stendi ya Msamvu na watalazimika kukaa kikao cha pamoja cha viongozi wote.

“Ushuru wa Masika na Msamvu tunasitishwa hadi tutakapokaa pamoja baina ya viongozi wa halmashauri ya Manispaa na madereva ili kuona tunatatua vipi ili shughuli ziweze kuendelea bila kuathiri watu wengine.”alisema Chonjo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa chama cha madereva Manispaa ya Morogoro, Michael Mongi alisema kuwa mgomo huo ni zao la viongozi wa Manispaa ya Morogoro kushindwa kuwashirikisha katika kupanga mambo yanayohusu usafiri wa daladala.

“Viongozi wa Manispaa yetu wamekuwa hawatushirikishi kwa lolote linalotuhusu sisi kama madereva na badala yake baadhi ya ushuru tumekuwa tukistukia asubuhi jambo ambalo siyo sahihi.”alisema Mongi.

Mongi alisema kuwa wao hawakatai kulipa ushuru isipokuwa mipango inayopangwa na Manispaa inapaswa kuwashirikisha ili waweze kutoa kero za kuboreshewa miundombinu ya barabara.

“Stendi ya Masika sasa hivi hakuna daladala inayoweza kuegesha gari kwa sababu tu katika maegesho pameweka vizuizi vya mawe na kujikuta madereva kuegesha gari juu ya stendi hiyo ambapo hulipia ushuru wa sh1000.”alisema Mongi.

Meneja wa Msamvu Properties Compan, Stanley Mhapa alisema kuwa suala la ushuru wa sh1000 kwa daladala zinazoingia ndani ya stendi ya daladala zitasaidia kampuni kuwezesha kurekebisha miundombinu katika kituo hicho.

Mhapa alisema kuwa ushuru wa Sh1000 unaolipwa kupitia madereva na makondakta hao wanalipaka kama wakala na anayestahili kulipa ni mmili wa daladala.

“Kuingia stendi ya daladala ya Msamvu ndani ni hiyari ya dereva na sio lazima kuingia katika stendi hiyo na madereva wana hiyari ya kushusha abiria kituo kimoja kabla ya stendi Msamvu ndani.”alisema Mhapa.

Mgomo huo ulisitishwa majira ya saa 5 asubuhi kwa madereva wa daladala hizo kuondoa magari yao eneo la langu kuu la kuingilia mabasi yanayoenda mikoani katika stendi hiyo huku ushuru wa Msamvu na Masika ukiwa katika mpango wa kuvutwa.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment
Millionaire  Ads