BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWAMUZI MCHEZO WA SOKA LIGI DARAJA LA PILI ATANDIKWA MAKONDE NA MASHABIKI MOROGORO

Mwamuzi wa kati kutoka Pwani, Gabriel Kinyogoli (mwenye mpira) na wasaidizi wake wakisindikizwa kutoka uwanjani na askari polisi baada ya mchezo baina ya wenyeji Sabasaba United na Namungo FC kumalizika, hali hiyo ilitokana na mwamuzi huo kutandikwa makonde na mashabiki wakimtuhumu kuipendelea timu ya Namungo iliyoshinda bao 2-0.

Juma Mtanda, Morogoro.
Mwamuzi wa kati kutoka mkoa wa Pwani, Gabriel Kinyogoli ameonja joto ya jiwe kwa mwaka mpya 2017 baada ya kushambuliwa na kutandikwa makonde mazito na mashabiki wa soka wakati wa mchezo wa ligi daraja la pili baina ya Sabasaba United FC na Namungo FC kwenye uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.

Mchezo huo ulimazika kwa Namungo FC ya mkoani Lindi kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya wenyeji Sabasaba United yaliyopatikana dakika ya 26 na dakika 55 na kupachikwa na Kulwa Hassan kwa kichwa.

Kipigo hicho kwa mwamuzi huyo wa kati kilitokana na mashabiki kumtuhumu kuipendelea timu ya Namungo FC kwa madai ya kutoa adhabu ya penalti iliyopelekea timu ya Sabasaba United kufungwa bao la kwanza dakika ya 26.

Adhabu hiyo ilitolewa baada ya mlinzi wa Sabasaba United, Omben Masawe kudaiwa kushika mpira eneo la hatari na kutoa penalti iliyopigwa na winga, Juma Kulachi na kufunga bao hilo.

Mwamuzi huyo alilalamikiwa na mashabiki hao kwa kushindwa kutoa adhabu ya penalti kwa Sabasaba United dakika ya 27 kufuatia mlinzi wa Namungo, Khamis Fakihi Dakika naye kudaiwa kushika mpira na mkono akiwa eneo la hatari baada ya shuti kali la mshambuliaji wa Sabasaba United, Iddi Gamba akiwa katika hekaheka za kufunga.

Tukio lingine lililowatia hasira mashabiki hao lilitokea dakika ya 38 baada ya kipa wa Namungo FC, Hamis Ogeja kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Sabasaba United, Iddi Gamba ambapo katika tukio hilo hakuweza kutoa kadi ya onyo kwa kipa ama mshambuliaji huyo.

Kutokana na matukio hayo mashabiki waliokuwa na jazba walijikusanya katika lango la kuingilia vyumbani na mwamuzi alipowakaribia alishushiwa makonde mfululizo kabla ya askari kumnasua kutoka kwenye kundi hilo la mashabiki.

Baada ya tukio hilo, ulinzi uliimarishwa wakati waamuzi hao wanaingia uwanjani kumalizia kipindi cha pili na baada ya mchezo huo kumalizika, askari kanzu na wenye sare iliwalazimi kutoa ulinzi mkali ili kuwanusuri na kipigo kutoka kwa mashabiki hao.

Msemaji wa timu ya Sabasaba United, Edward Sebastian akizungumza na MTANDA BLOG alisema kuwa kupigwa kwa mwamuzi huyo, Gabriel Kinyogoli kimetokana na jazba kutoka kwa mashabiki wa soka hasa mwamuzi kudai kufumbia macho matukio yaliyopaswa kutoa adhabu.

“Mwamuzi alikuwa na matokeo yake mfukoni, tumeshuhudia mlinzi wetu ameweka mpira kifuani lakini mwamuzi ameamuru ipigwe penalti tumekubali, mbona mlinzi wa Namungo jezi no 14 (Khamis Fakihi) ameshika mpira mkononi na mwamuzi hajatoa adhabu ya penalti.?alihoji Sebastian.

Kwa upande wa Kocha mkuu wa timu ya Namungo FC, Zulkifri Mahadi alisema kuwa amefurahishwa na ushindi huo na wanajipanga dhidi ya Might Elephat FC ya Songea katika uwanja wa Sabasaba mjini Nachingwea januari 7.

Kutokana na matokea hao Namungo FC inaongoza kundi lake ikiwa na pointi 12 wakati Might Elephat FC ina pointi 11, Mawenzi FC ikiwa na pointi nane na Sabasaba United ikiyumba na pointi zake sita.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: