BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAMBO YAWA MAGUMU KWA MBUNGE WA JIMBO LA ARUSHA MJINI, AENDELEA KUSOTA MAGEREZA


HATIMA ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema sasa iko mikononi mwa Mahakama ya Rufaa baada ya jana mawakili wa serikali kuwasilisha maelezo ya notisi ya kukusudia kukata rufaa kupinga mbunge huyo kupewa dhamana.

Msuguano wa kisheria kati ya mawakili wa Lema na wa serikali umedumu kwa zaidi ya miezi miwili sasa huku kila upande ukipinga uamuzi ya upande mwingine.

Mawakili wa serikali waliwasilisha notisi hiyo iliyosajiliwa Desemba 30, mwaka jana katika masjala ya Mahakama ya Rufaa Kanda ya Arusha na itapangiwa tarehe katika vikao vya mahakama hiyo vinavyokaa mara tatu kwa mwaka.

Lema alikamatwa mjini Dodoma Novemba 2, mwaka jana na kufikishwa mahakamani Novemba 8 mwaka huo huo kwa mashitaka ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

Alinyimwa dhamana na kurudishwa mahabusu katika Gereza la Kisongo lililopo nje kidogo ya Jiji la Arusha. 


Jana Jaji Salma Magimbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, alitarajiwa kusoma uamuzi wa ama kumpa Lema dhamana au la, kufuatia ombi la notisi ya kupinga dhamana lililowasilishwa na mawakili wa Serikali mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Desderi Kamugisha, Novemba 11 mwaka jana.

Katika ombi hilo, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Paul Kadushi, aliwasilisha notisi ya kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga Lema kupewa dhamana, ombi ambalo alilitamka muda mfupi kabla ya Hakimu Kamugisha kutoa masharti ya dhamana.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: