BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE PETER LIJUALIKALI BADO NI MBUNGE HALALI WA JIMBO LA KILOMBERO LICHA YA KUFUNGWA JELA

 

Tukio la mbunge wa Kilombero Peter Ambrose Lijualikali kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela na Mahakama ya wilaya ya Kilombero kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero, mbunge huyo ataendelea kuwa mbunge halali.

Kutokana na hukumu hiyo kumeibuka mi
jadala mbalimbali na kushika kasi hasa katika mitandao ya kijamii, mitaani  na kila mahali baada ya

 Lijualikali ambaye alikuwa mshtakiwa namba moja alipewa adhabu hiyo huku mshtakiwa namba mbili, Stephano Mgata (35) wakitenda kosa hilo Machi 1, 2016 majira ya saa 4 asubuhi nje ya ukumbi wa kikao cha Baraza la Madiwani katika eneo la Kibaoni halmashauri ya wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro.

Vifungu namba 89 kifungu kidogo cha kwanza B, cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 ndivyo vilivyotumika kuwatia hatiani licha ya katika utetezi washtakiwa walikana mashtaka na hivyo kufanya kesi kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na upande wa mashtaka ukathibitisha bila kuacha shaka. 


Akizungumza katika mahojiano katika kituo cha Luninga cha TBC One, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramadhan ameeleza kuwa, Lijualikali ataendelea kuwa mbunge katika jimbo hilo.

Kailima alisema kuwa mbunge huyo ataendelea na wadhifa wake kwa kuwa sheria inasema ili kupoteza kiti ni lazima uwe umepewa adhabu ya kifungo cha zaidi ya miezi sita jela tofauti na yeye aliyefungwa chini ya hapo.
Akifafanua zaidi Kailima alisema kuwa katika Ibara ya 67(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza mambo yanayotoa sifa ya kuwa Mbunge kutoka madarakani ni kifungo cha zaidi ya miezi sita jela. 


"Hakimu amemhukumu Lijualikali kifungo cha kwenda jela miezi sita kwa hiyo bado hajapoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge akiwa gerezani na baada ya kumaliza kifungo chake ataendelea na wadhifa wake wa ubunge."alisema Kailima.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: