BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Millionaire  Ads

MOROGORO, KAGERA NA MBEYA KWAIBUKA MATUKIO YA KUTISHA KWA WATU KUFUKUA MAKABULI WALIPOZIKWA MAITI ZA ALBINO.WAKATI matukio ya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi yakipungua katika maeneo mbalimbali nchini, hali imebadilika na sasa watu wameanza kufukua makaburi ya albino hao.

Akizungumza katika semina inayofanyika jana jijini hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Under The Same Sun (UTSS) Tanzania, Vicky Mtetema, alisema matukio matatu ya ufukuaji makaburi yametokea mwezi huu katika mikoa ya Kagera, Morogoro na Mbeya.

Pamoja na matukio hayo, Mtetema alisema kutokana na jitihada za shirika hilo, kumekuwa na mafanikio makubwa ya kupungua kwa vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi na elimu inayotolewa imesaidia kuwapa watu uelewa na maana halisi ya ‘albinism’.

Alibainisha kuwa kumbukumbu zinaonyesha tukio la kutumia viungo vya watu wenye ualbino lilianza mwaka 2007 kwa kufukuliwa kaburi, lakini baadaye matukio ya kukata viungo yakaanza kwa kasi.

Mtetema alisema wameamua kutoa semina ambayo ni ya kwanza na imeanzia mkoani Mwanza kwa Kanda ya Ziwa ili kutoa elimu ya uelewa juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi, na jinsi ya kuishi nao kwa sababu takwimu zinaonyesha asilimia kubwa ya vitendo vya kikatili hutokea katika kanda hiyo.

Alionyesha pia wasiwasi kwa nchi jirani kuwa na uhusiano na Tanzania wa kununua viungo vya albino kwa kuwa hata ufukuaji wa makaburi hayo ni jambo lililoanzia nje ya nchi.

Semina hiyo ya siku nne imelenga kutoa elimu kwa watu kutoka sekta mbalimbali ili elimu wanayoitoa iwawafikie watu wote na rika zote kwa ajili ya kupunguza kama si kumaliza kabisa mauaji na matendo ya kikatili katika jamii. 


Elimu hiyo inatolewa juu ya watu waliopatwa na simanzi hasa wazazi, jamaa, ndugu na marafiki ambao wamekumbana na matukio hayo katika familia zao huku jamii ikitakiwa kuwa mabalozi wazuri mahali popote wanapokwenda, juu ya watu wenye ulemavu.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment
Millionaire  Ads