BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI WAJISABABISHIA KUNYIMWA USHIRIKIANO KUTOKA KWA WANANCHI

MWAMKO mdogo wa wananchi katika kulisaidia Jeshi la Polisi umeelezwa kuwa ndiyo changamoto kubwa inayosabisha kusuasua kwa upelelezi wa makosa ya jinai.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Nipashe jijini, Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Boaz, alisema wananchi wanakosa mwamko wa kutoa taarifa za uhalifu kwa polisi.

Kamishna Boaz alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wagumu kuisadia polisi kwa madai kuwa jeshi hilo halitunzi siri za watoa taarifa, hivyo kuwataja kwa wahalifu.

"Msingi mkubwa wa intelijensia na uwezo wake ni pale inapokuwa na uwezo wa kupata taarifa nyingi," alisema Boaz. 


"Kwa nchi zilizoendelea, mtu akiona jambo anaweza kutoa taarifa, lakini hapa kwetu linaweza kutokea jambo kubwa kabisa lakini ukiwauliza (watu), hakuna aliye tayari kuzungumza."
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: