Wasanii Wema Sepetu na Steve Nyerere katika picha ya maktaba.
Trim Saleem, amekuwa akizungumzia masuala yanayojitokeza hasa ya wasanii kwa undani zaidi katika ukurasa wake wa facebook kwa mambo ya tasnia ya filamu, muziki na n:k leo amedokeza suala la Steve Nyerere na Wema Sepetu.
Steve Nyerere ambaye ni kada wa CCM afunguka haya kuhusu Wema Sepetu na Mama Wema.
Kati ya wasanii waliolipwa fedha nyingi na CCM ni dada (Wema Sepetu), na hakuna msanii wa Mama Ongea na Mwanao anayeidai CCM-Steve Nyerere.
CCM tulifanya kampeni na tulilipwa, hatukuingia mkataba kuwa baada ya kampeni ukikamatwa na unga, CCM itakulinda na kukutetea- Steve Nyerere.
Si kweli kuwa nilishinikiza wabunge wamjadili Wema, nilitumia sanaa tu kumlaghai Mama Wema atulie kuhusu Wema kukamatwa- Steve Nyerere.
Si kweli kuwa nilishinikiza wabunge wamjadili Wema, nilitumia sanaa tu kumlaghai Mama Wema atulie kuhusu Wema kukamatwa- Steve Nyerere.
Sijazungumza na Waziri yeyote kuhusu Wema kukamatwa, nilitaka kumtuliza Mama. Ni kama kumlaghai mtoto na pipi achomwe sindano- Steve Nyerere.
Niwaombe radhi wote niliowataja katika mazungumzo yangu, sikufanya kwa nia mbaya, nilitaka kukilinda chama na kumsaidia Wema- Steve Nyerere.
Niliombe radhi Bunge tukufu, nimuombe radhi Spika Ndugai kwa kudanganya kuwa nilishinikiza Wabunge wamjadili Wema Sepetu- Steve Nyerere.
Nimuombe radhi Rais Magufuli kwa kuwatumia Mawaziri wake aliowaamini katika hili, lakini sikufanya kwa nia mbaya- Steve Nyerere.
Kama wanadhani nitahama nao, wamepotoka. Hata kama ni kuhama, mimi nitakuwa msanii wa mwisho kuhama CCM- Steve Nyerere
0 comments:
Post a Comment